01/09/2026
Mahak**a ya Wilaya ya Clark County, nchini Marekani imemkuta Duane “Keffe D” Davis na hatia ya kuhusika katika mauaji ya mwanamuziki maarufu wa rap, Tupac Shakur, aliyeuawa miaka 30 iliyopita katika shambulio la lililotokea kwenye gari huko Las Vegas.
Katika sh*taka hilo majaji walijadiliana kwa muda usiozidi saa tatu kabla ya kumkuta Davis, mwenye umri wa miaka 63, na hatia ya mauaji kwa kutumia silaha hatari, huku kosa hilo likihusishwa na nia ya kukuza, kuendeleza au kusaidia shughuli za genge la kihalifu.
Jaji wa Mahak**a ya Wilaya ya Clark County, Carli Kierny, ameweka tarehe Oktoba 13, 2026 kuwa siku ya Davis kusomewa adhabu yake rasmi na ikumbukwe kuwa Davis anakabiliwa na adhabu ya juu kabisa ya kifungo cha maisha jela.
Tupac Shakur aliuawa kwa kupigwa risasi katika shambulio la gari kwa gari huko Las Vegas mwaka 1996, na kifo chake kimeendelea kuwa miongoni mwa kesi zinazozungumziwa zaidi katika historia ya muziki wa hip-hop.
Chanzo ABC News
✍️:
31/08/2026
, (🏟 Villa Park, Birmingham)
FT: Astonvilla 0️⃣-1️⃣ Arsenal
⚽️ B. Saka 59'
31/08/2026
, (🏟 KaitabaStadium)
FT: Kagera Sugar ️0️⃣-2️⃣ Azam FC
⚽️ Zidane Sereri 16'
⚽️ Feisal Salum 22'
31/08/2026
Mwaka 2009, mtangazaji wa CBS Katie Couric alifanya mahojiano na Rapa Lil Wayne ambaye mahojiano yake yalizua taswira mseto kuhusu maisha na namna ya kuishi kwa mtu binafsi na jamii.
Katika maswali yake Couric alimuuliza Lil Wayne ikiwa anajiona k**a yeye mfano mzuri wa kuigwa, na jibu lake likawa hivi;
"Mimi si mfano wa jinsi watu wanavyopaswa kuishi maisha yao. Kamwe katika maisha yangu nisingejitokeza kuwa mfano kwa watu wa jinsi ya kuishi maisha yao. K**a unahitaji mfano wa jinsi ya kuishi, basi hukupaswa hata kuzaliwa. Moja kwa moja (Straight up). Mimi ni mfano bora wa kuigwa, kwa sababu mimi ni mfano wa kuigwa kwa watu wawili tu, na hiyo ndiyo yote. Hicho ndicho chenye maana kwangu hao wawili. Hivyo kwa nini usihangaike na wako, na uwache wao wahangaike na wa kwao? Mimi nina wa kwangu." Alisema Lil Wayne.
Je, na wewe ni mfano wa kuigwa..........??
31/08/2026
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linawashikilia askari wake sita kwa tuhuma za kuhusika katika mauaji ya kijana mwenye umri wa miaka 23, Katibu Kigaduso, mfugaji kutoka jamii ya Kimang'ati na mkazi wa Kijiji cha Bwakila Chini, Kata ya Bwakila Chini, Halmashauri ya Morogoro.
Kwa mujibu wa K**anda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi wa Polisi Andrew Kantimbo amesema askari hao sita wanashikiliwa wakati uchunguzi ukiendelea ili kubaini mazingira ya tukio hilo na kuwachukulia hatua zaidi.
31/08/2026
Kiungo wa Kimataifa wa Tanzania, Alphonce Mabula Msanga ametambulishwa rasmi k**a mchezaji mpya wa klabu ya JS Kabylie ya Nchini Algeria kwa uhamisho huru baada ya mkataba wake na klabu ya Şamaxı FK ya Azerbaijan kusikia ukomo.
Klabu hiyo imethibitisha kukamilisha usajili wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 leo Agosti 31, 2026 kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii bila kuweka wazi urefu wa mkataba wake klabuni hapo.
31/08/2026
Kwa mujibu wa The Athletic ni kwamba uhamisho wa Cody Gakpo kuelekea Manchester City umeshindikana baada ya Liverpool FC kukataa dau la hadi pauni milioni 80 kutoka Manchester City waliokuwa wakimuhitaji zaidimchezaji huyo.
City sasa wameelekeza nguvu zao zote katika kujaribu kumsajili Enzo Fernandez kutoka Chelsea, ambaye wamekuwa wakimvizia msimu wote huu wa kiangazi.
31/08/2026
, (🏟 Meja JeneraliIsamuyo)
FT: Simba SC 2️⃣-0️⃣ Geita Gold FC
⚽️ Chama Clatous 22'
⚽️ Libase Gueye 58'
31/08/2026
Msimu wa kwanza nyota Cristiano Ronaldo aliporejea Manchester United mwaka 2021 alicheza Mechi18 Mabao 3 Pasi za mabao (Asisti)
✅️Mabao 24 katika mashindano yote🎯 ✅️Pasi 3 za mabao zilizochangia ushindi
✅️Tuzo mbili za Mchezaji Bora wa Mwezi wa ✅️Ligi Kuu ya Uingereza (Premier League)
✅️Tuzo ya Bao Bora la Mwezi
✅️Wa tatu kwa ufungaji bora EPL
✅️Miongoni mwa Kikosi Bora cha Msimu EPL
31/08/2026
Nyota Lionel Messi ametangaza rasmi kustaafu kucheza soka la kimataifa akiwa na timu ya taifa ya Argentina.
Messi ametangaza uamuzi huo leo, Agosti 31, 2026, kupitia ujumbe aliouchapisha katika Mitandao ya Kijamii, akisema ni uamuzi unaomuuma lakini anaamini wakati umefika wa kufunga ukurasa wake akiwa na Timu ya Taifa.
“Baada ya muda huu kupita tangu fainali na baada ya kufikiria sana, nataka kuwaambia wote kwamba nimeamua kustaafu kuitumikia Timu ya Taifa, ulikuwa uamuzi ambao uliumiza na bado unaumiza moyoni, lakini ninaelewa kwamba huu ndio wakati,” amesema Messi.
“Nimetoa kila kitu, sina zaidi cha kutoa, na pia kuna Vijana wenye uwezo mkubwa wanaokuja ambao wanastahili kupata nafasi,” amesema Messi.
Flowin vitus