Watani wa Jadi

Call Directions Website

Watani wa Jadi Official Page ya Watani wa Jadi. Habari zote Exclusive za Yanga na Simba utazipata hapa 24/7. Hii ni Official Page ya Watani wa Jadi kwenye Mtandao wa Facebook.

Habari zote Exclusive kutoka kwenye klabu za Yanga na Simba utazipata hapa muda wote 24/7
Habarika na Sisi

Baada ya siku takribani nane za mapumziko, Yanga SC imerejea uwanjani na kuanza tena safari ya maandalizi kuelekea mchez...
30/09/2026

Baada ya siku takribani nane za mapumziko, Yanga SC imerejea uwanjani na kuanza tena safari ya maandalizi kuelekea mchezo ambao tayari umeanza kuteka hisia za mashabiki—Kariakoo Derby dhidi ya Simba SC.

Kikosi kimeanza kurejesha kasi baada ya mapumziko ya FIFA, huku benchi la ufundi likiwa na jukumu la kukiweka kikosi katika hali bora kabla ya Oktoba 10, siku ambayo macho ya soka la Tanzania yataelekezwa Uwanja wa Uhuru.

Sasa hakuna tena likizo. Mazoezi yamerudi, ushindani wa nafasi unaanza upya na hesabu za dabi zinaingia mezani.

Simba nao wamekuwa kambini Afrika Kusini wakati wa mapumziko ya FIFA, hivyo maandalizi ya pande zote mbili yanaendelea kuelekea pambano hilo.

10/09/2026

Kuelekea mchezo wa pili wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Young Africans (Yanga SC), Ali Kamwe, ameeleza namna klabu hiyo ilivyojiandaa kwa mchezo huo huku akifafanua yaliyotokea katika mchezo wa kwanza nchini Botswana.

Kamwe amesema Yanga imeendelea kufanya maandalizi yake kwa umakini mkubwa, ikitambua umuhimu wa mchezo huo katika safari yake ya kuwania nafasi ya kuendelea na hatua inayofuata ya mashindano hayo ya CAF.

Akizungumzia mchezo wa kwanza uliochezwa Gaborone, Kamwe ameeleza mazingira ambayo timu ilikutana nayo nchini Botswana, pamoja na namna kikosi kilivyokabiliana na changamoto hizo ili kupata matokeo yaliyowekwa kwenye kumbukumbu.

Wakati jina lake likizidi kutawala mijadala ya soka nchini, hasa kuhusu historia yake na Yanga SC, kiungo mshambuliaji w...
10/09/2026

Wakati jina lake likizidi kutawala mijadala ya soka nchini, hasa kuhusu historia yake na Yanga SC, kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Clatous Chama, ameamua kuweka mstari mmoja wazi — mambo ya nje ya uwanja hayana nafasi kwenye akili yake.

Chama amesema hayo katika tukio la Simba Media Day lililofanyika MO Arena, Bunju jijini Dar es Salaam, akisisitiza kuwa uzoefu wake wa muda mrefu katika soka umemjengea uwezo wa kutenganisha kelele za nje na kazi yake ya ndani ya uwanja.

Kwa mujibu wa Chama, mjadala wowote unaoendelea nje ya uwanja hauwezi kumtoa kwenye mstari wa majukumu yake akiwa na Simba.

“Mimi ni mchezaji mzoefu, hayo masuala ya nje ya uwanja hayawezi kunisumbua. Akili na mawazo yangu yako kwa klabu ya Simba ambayo mimi na wenzangu tunawajibika katika kuhakikisha tunafikia malengo,” alisema Chama.

Kauli hiyo imekuja baada ya Chama hivi karibuni kufichua mambo yaliyomkuta wakati akijiunga na Yanga, akisema kuwa haikuwa dhamira yake ya awali kuhamia klabu hiyo, lakini mazingira yaliyokuwepo wakati huo yalimlazimisha kufanya uamuzi huo.

Chama alikwenda mbali zaidi kwa kueleza kuwa kipindi chake Yanga hakikuwa na furaha kwake, kauli iliyofungua ukurasa mpya wa mjadala miongoni mwa mashabiki wa Simba na Yanga.

Lakini sasa, baada ya kurejea Simba, Chama anaonekana kutaka kuacha kila kitu nyuma na kuzungumza kupitia miguu yake ndani ya uwanja.

Akiwa sehemu ya wachezaji muhimu katika kikosi cha Simba, macho ya mashabiki sasa yameelekezwa kwake kuona k**a atatumia ubora wake kujibu kila mjadala unaoendelea nje ya uwanja.

Mjadala ni wa nje. Kazi ya Chama ni ndani ya uwanja. Na yeye mwenyewe tayari amesema akili yake ipo Simba.

Baada ya kufanyiwa tathmini maalum ya kitabibu nchini Afrika Kusini, Clement Mzize na Dickson Job wameonekana kuwa katik...
08/09/2026

Baada ya kufanyiwa tathmini maalum ya kitabibu nchini Afrika Kusini, Clement Mzize na Dickson Job wameonekana kuwa katika hali nzuri na sasa wako tayari kuanza safari ya kurejea uwanjani.

Nyota hao waliondoka na kikosi cha Yanga kuelekea Botswana, lakini walibaki Afrika Kusini kwa ajili ya vipimo vya mwisho kuhusu maendeleo ya majeraha yaliyokuwa yamewaweka nje ya uwanja.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe, amethibitisha habari hiyo njema huku akitoa ujumbe ambao bila shaka utaongeza hamasa kwa mashabiki wa Yanga:

“Kimsingi, wachezaji hawa wawili ni k**a usajili mpya kwetu. Wale ambao mmecheza na Yanga na hamkukutana na Clement Mzize Bull Striker, basi niwaambie tu kwamba Mzize na Job wamerudi.”

Mzize, ambaye amekosekana kwa takribani msimu mzima, sasa yuko mlangoni kurejea na kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji.

Job, ambaye alipata jeraha mwezi Machi katika mchezo dhidi ya Simba uliochezwa New Amaan Complex, naye sasa yuko tayari kuanza ukurasa mpya.

Kwa kifupi, Yanga haijasajili mtu sokoni, lakini imepata wachezaji wawili muhimu!

Kinachobaki sasa ni suala la muda kabla ya mashabiki kumuona tena Clement Mzize “Bull Striker” na Dickson Job wakivaa jezi ya Yanga uwanjani.

08/09/2026

UJUMBE KUTOKA KWA JEMEDARI SAIDI

04/09/2026

Kuelekea mchezo wa kesho wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali, Kocha Mkuu wa Yanga SC amezungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya kikosi chake pamoja na namna anavyokiona kikosi cha Gaborone United.
Kocha huyo amesema wanafahamu ubora na uwezo wa wapinzani wao, hivyo wamejiandaa kwa umakini mkubwa kuhakikisha wanaingia uwanjani wakiwa tayari kupambana kwa dakika zote 90.
Amesisitiza kuwa mchezo huo hautakuwa mwepesi, huku akiwataka wachezaji wake kuzingatia mipango ya kiufundi na kutumia nafasi zitakazojitokeza ili kupata matokeo mazuri katika mchezo huo wa kwanza.
Yanga inatarajia kukutana na Gaborone United kesho, Jumamosi, Septemba 5, 2026, jijini Gaborone, Botswana, katika hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mshambuliaji wa Singida Black Stars, Jonathan Sowah, amefunguka kwa mara ya kwanza kwa kina kuhusu kilichotokea wakati w...
03/09/2026

Mshambuliaji wa Singida Black Stars, Jonathan Sowah, amefunguka kwa mara ya kwanza kwa kina kuhusu kilichotokea wakati wa kipindi chake ndani ya Simba SC, akisema alijikuta katika mazingira ambayo hakuwa na uwezo wa kuchagua zaidi ya kufanya kile alichoelekezwa.

Sowah amesema bado huwa anajisikia vibaya anapokumbuka namna mambo yalivyokwenda, akisisitiza kuwa alifika Tanzania kwa ajili ya kutafuta mafanikio na kufanya kazi yake k**a mchezaji.

“Kuna wakati huwa najisikia vibaya, kile kilichotokea sikuwa na namna wala sikuwa na chaguo lolote. Nilikuja huku kutafuta pesa, nilipaswa kufanya kile wanachotaka nifanye.”

Mghana huyo pia amedai kuwa kabla ya kuondoka Simba, alikuwa katika kiwango kizuri licha ya changamoto alizokuwa akikabiliana nazo. Kwa mujibu wake, alicheza mechi nne na kufunga mabao matatu, wakati huo akiona ushindani wa nafasi ya ushambuliaji ndani ya kikosi.

“Kabla ya kuondoka Simba nilicheza mechi nne nikafunga magoli matatu na walikuwa wanahangaika na washambuliaji wanaowaamini.”

Sowah ameendelea kusisitiza kuwa kufunga mabao ni sehemu ya uwezo wake wa asili, akijitaja k**a ‘goal poacher’ na kusema hana hofu kuhusu uwezo wake wa kuzifumania nyavu.

Lakini kauli yake nzito zaidi imekuja kuhusu maelekezo ya kufanya mazoezi na timu ya vijana ya Simba.

“Simba told me to train with the U-20 team and I refused because there were no U-20 issues in my contract. I am a national team player, I can't play with kids. Can they tell Kagoma to play U-20 when he's a national team player?”

Kauli hizo zimeibua maswali kuhusu sababu zilizofanya safari yake Simba ifike mwisho, huku Sowah akionekana kutaka kuweka wazi upande wake wa kile kilichotokea.

Clement Mzize na Dickson Job wameondoka Dar es Salaam pamoja na msafara wa Yanga ulioelekea Botswana, lakini safari yao ...
02/09/2026

Clement Mzize na Dickson Job wameondoka Dar es Salaam pamoja na msafara wa Yanga ulioelekea Botswana, lakini safari yao imeishia kwa muda Johannesburg, Afrika Kusini, ambako nyota hao wamebaki kwa ajili ya uchunguzi wa afya.
Yanga inaelekea Botswana kwa ajili ya kuikabili Gaborone United katika mkondo wa kwanza wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, mchezo ukipigwa Jumamosi, Septemba 5, saa 2:00 usiku kwa saa za Tanzania.
Kwa mujibu wa Ali Kamwe, hakuna haraka ya kuwarejesha uwanjani Mzize na Job bila kwanza kuthibitisha hali zao za kiafya.
Wawili hao wamefanyiwa uchunguzi katika hospitali walikofanyiwa upasuaji awali, huku majibu ya vipimo yakitarajiwa kutoa picha k**a wako tayari kurejea kwenye majukumu ya ushindani.

Ikiwa watathibitishwa kupona kikamilifu, basi mashabiki wa Yanga wanaweza kuanza kutazamia kurejea kwa nyota hao kikosini.

02/09/2026

Chuma amekuja na Semina Elekezi..!!

01/09/2026

Kuelekea mchezo wa kwanza wa kimataifa wa dhidi ya Gaborone United ya Botswana, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ali Kamwe, ametoa kauli kuhusu maandalizi na mtazamo wa Yanga kuelekea mchezo huo.
Kamwe amezungumzia hali ya kikosi, maandalizi pamoja na namna Wananchi wanavyouangalia mchezo huo wa kwanza wa hatua ya kimataifa.

Address

Dar Es Salaam
255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Watani wa Jadi posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share