16/11/2019
Deo Kanda yule mtu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, yule fundi mmoja kutoka viunga kwa Kamarondo pale Lubumbashi
Deo kaja Tanzania kuchukua nafasi ya Prince wa Msimbazi, kipenzi cha wanasimba Immanuel Okwi, tafsiri ya haraka na ukubwa wa jina lake ni wazi tulifahamu viatu vitamtosha haraka
Kocha wake Lamine N'diaye alimuhusudu sana, ile TP iliyojaa mafundi wa kila rangi mtu wangu, ila Deo alicheza, ujio wake hapa Bongo sikutarajia makubwa, naona k**a upepo umekata sana
Sio lazima sana Mzamiru acheze k**a Mbenza Bedi yule, sio lazima Shiboub acheze k**a Dioko Kaluyituka yule, sio lazima pacha wake awe Ngandu Kasongo yule au Given Singuluma, ni wazi ameshuka sana Deo
Kuna vitu vya kiufundi labda vinamtatiza, Deo pale Lubumbashi walimtumia mara nyingi k**a Forward na k**a anacheza pembeni ni k**a wide forward, ila kwa Simba naona kuna Meddie eneo hilo, lazima operation ya Deo iwe chini
Mbaya zaidi kucheza pembeni kasi yake haiendani na Mohamed Hussein, MO anataka upepo wa winga muda wote, Deo alienjoy TP alipokuwa na Kiritsho Kasusula, walielewana sana kwakua pumzi zilikuwa leveled, ila sasa kuna disparity kubwa sana kati yake na leftback wake
Kwa hype aliyonayo sasa naona atastruggle ndani ya Simba, mfumo unahitaji pumzi, vision na utulivu, Deo ana skills sana, ila kuna wakati modern football inataka unyumbufu wa kimfumo, kuna wakati unamwona mwili unataka ila akili haitaki
Huenda ikawa ramli chonganishi 😁😂ila frankly speaking Deo hakupaswa kuja sasa kwenye Simba hii na aina yake ya game, k**a Deo angekuwa beki nisingekataa ila kwenye eneo lake linataka extra potentials, which yeye kwasasa muda umeenda sana
Miraji Athuman, Hassan Dilunga na Rashid Juma wanaweza kufanya anachofanya na zaidi, so bad for him, so bad for him, Deo cool down yoh, time is up
31/08/2019
Tulikubaliana hapa kuwa Manchester United haipaswi kumtimua Kocha wake kwakuwa karithi kundi la wachezaji wengi ambao jezi ya United ni kubwa kwao, hivyo aendelee kuwatoa nje taratibu kwakuwa ni kazi kuwatoa wote kwa pamoja, k**a alivyoanza kwa Smalling na Mateo.
.
Dirisha la January atoe tena wengine, kisha aongeze wazuri wengine hii ijirudie kwa misimu k**a miwili ijayo alafu msimu wa 2022/23 naamini watapata United wanayotaka.
Tuk**alizia na Chelsea kuwa bado wana ile Second half syndrome, haka kaugonjwa kanawaumiza sana, wanapaswa kulipatia tiba, mwalimu aongeze zaidi nguvu kwenye physical fitness, ile nishati inayotumika kipindi cha kwanza ni kubwa mno ile high pressing! Si kamwona Klopp kaachana na Gegen Pressing kaja na High Line play na Low pressing, NISHATI NI MUHIMU
Basi kikao kikafungwa hivyo kwenye WEEKEND SPORTS ya KISS FM TANZANIA na wajumbe wote tutakutana tena kesho.
30/08/2019
JAMES KOTEI NDANI YA KIVULI CHA MNYAMWEZI MMOJA MLOWEZI WA NG'AMBO, KEARYN BACCUS 'THE MOZART'
✨Kiungo wa mpira, eneo la dimba la juu na chini ndani ya Kaizer Chiefs 'Amakhosi' Muastralia mmoja KEARYN BACCUS, jamaa anampa kocha machaguo ya kutosha ndani ya kikosi, huyu ndie anamnyima usingizi kiungo Mghana James Kotei ndani ya PSL.
Baccus ni mtaalamu wa Link up play, anadetect tempo, playmaker mzuri, anafika mguuni na anafunga pia, huyu ni versatile player, kifupi ni Hybrid wa viungo vyote vitatu (holding, playmaking na attacking midfielder), ndani ya mchezo we muite tu ataitika na atakuja kukupa utakacho kocha.
✨Baccus anaishi Durban ndani ya nchi ya Nelson Rohlhla Madiba Mandela, amezaliwa 1991 jijini humo ila ana uraia wa Australia akiwa amecheza timu k**a Perth Glory, Western Sidney na Melbourne City za Australia kabla ya kujiunga na Amakhosi, 2019 huku mkataba ukiisha 2022.
Chiefs wana viungo wengi wenyw ubunifu kwa kiasi ambacho wamekuwa wakishinda game nyingi kwenye eneo hilo 'power house', akisaidiana na George Maluleka, William Katsande na Lebogang Manyama, hakika kocha Ernst Duddendorp hana kazi nzito.
James Kotei atacheza muda ukifika, atapata namba ila afanye kazi ya ziada, Amakhosi wamejaa kwenye kiungo yabidi aendelee kusubiri.
29/08/2019
SANIBONANI! 👋SIKHONA, SIYABONGA NINA NINJANI?!.. NAWASALIMU KWA KIZULU WANANGU WA GHETTO KISHA TWENZETU KWA NAHODHA LUCAS VALERIU NTUBA RADEBE 'RADEBEER'.
✨Zama zile za ubaguzi wa rangi 'Apartheid Regime' bondeni kwa Madiba 🇿🇦, 1969 ndani ya mitaa ya Diepkloof maeneo ya SOWETO enzi za uongozi wa Waziri Mkuu Balthazer Johannes Vorster, ni mwaka huo anazaliwa fundi huyo wa Mpira.
Radebe alipelekwa mbali na mitaa ya SOWETO kutokana na ubaguzi wa rangi kuzidi na mauaji mbalimbali ikiwemo Soweto Massacre na Sharpville Massacre, hivyo akapelekwa Bophuthatswana kuepuka majanga hayo.
✨Radebe alianza soka k**a Golikipa kisha akaenda eneo la kiungo na mwisho akaenda kucheza beki ya kati na hapo ndipo akapata umaarufu mkubwa.
Amecheza ICL Birds, Wolf Wanderers, Kaizer Chiefs na Leeds United, wakati Radebe anakaribia kuhama Chiefs alipigwa risasi na mtu asiyejulikana na mpaka leo haijulikani sababu ni nini.
Mitaa ya SOWETO inamfahamu Lucas k**a beki mkatili mwenye roho mbaya, mwenye mabao ya acrobatic scissor kicks, diving headers na man marking (mtu na mtu).
✨1994 Radebe anaelekea Leeds United kuungana na Mnyama mmoja Philemon Masinga 'Chippa' na kwa pamoja walikuwa wanaitwa 'Homeboys' ndani ya Yorkshire, ardhi ya malikia.
Radebe alipewa unahodha wa Leeds United chini ya kocha George Graham, mitaa ya Yorkshire ilipagawa mno, walimpa majina k**a 'Rhoo' 'Chief' na baadae wakatengeneza bia na kuita 'Radebeer'.
Ameitumikia timu ya taifa 'Bafana Bafana' kwa mafanikio makubwa alikuwepo 1996 wanatwaa Ubingwa wa Afrika, alikuwepo 1998 & 2002 kombe la dunia pia.
Nimeandika tu kujisikia k**a siku ntakavyojisikia kumwandika Mark Fish, Helman Mkhalele, Shoes Moshoueu, David Nyathu, Doctor Khumalo na Shaun Bartlett, mafundi mno na ni watu sana.
⚠Wenyewe Kaizer Chiefs wanamkumbuka mtu huyu, mitaa inakumbuka shughuli yake! Kubonga Mina, Sa la kahle Lucas 'Rhoo' Radebe!.
@ Kariakoo, Dar es Salaam