Global Foot

Global Foot

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Global Foot, Sports Event, Osofia, Kigoma.

Msafiri Sports Hub | Taarifa Moto za Michezo
⚽️ Habari, Matokeo & Takwimu
🌍 EPL | La Liga | Serie A | Bundesliga | Ligue 1 | NBC
🔥 Hashtags #MsafiriSports #FootballUpdates
📲 Matukio Mubashara & Uchambuzi

KWA MATANGAZO KARIBU
PIGA 0756170880

12/05/2026

Wakala wa FIFA kutoka nchini Uganda, Ronnie Santos Mwine Fred ameripoti kuwa, Maskauti wa vigogo wa 🇹🇷Uturuki Fenerbahçe SK wamekuwa 🇹🇿Tanzania kwa siku ya 4 sasa, na sababu pekee ni nyota kijana wa timu ya taifa ya 🇺🇬Uganda "The Cranes" Allan Okello!
Na Watamfuatilia tena katika mchezo ujao dhidi ya Dodoma Jiji.

Katika mechi ya kwanza waliyomtazama, alifunga mabao 2 na kutoa assist 1 dhidi ya Coastal Union

Young Africans S.C. wanatajwa kuhitaji takribani dola milioni 3 (Tsh 7.8B) kwa nyota huyo wa timu ya taifa ya Uganda, The Cranes.

09/05/2026

Mwaka 2005, Peter Crouch alipojiunga Liverpool, alitumia wiki yake ya kwanza akiishi hotelini ambapo alimpenda kimyakimya mmoja wa wahudumu wa mapokezi (receptionist).

Akiwa mazoezini, hakuweza kujizuia kumzungumzia mwanamke huyo kwa wachezaji wenzake wapya, akieleza jinsi alivyokuwa mrembo na jinsi alivyofikiri ana nafasi ya kumpata.

Hapo ndipo Jamie Carragher alipowaita wachezaji wote na kumwambia Crouch arudie alichokuwa akisema.
Kwa kujiamini, Crouch aliendelea kumsifia, akidiriki hata kukiri kuwa alikuwa akimfikiria mwanamke huyo kutwa nzima.

Kisha likaja tukio lililopindua kila kitu.
Mhudumu huyo wa mapokezi… kumbe alikuwa ni mke wa mchezaji mwenzake mpya, Xabi Alonso. 🤣

Wachezaji wote waliangua kicheko baada ya kubaini hilo...

01/05/2026

Ulianza kuangalia Kombe la Dunia mwaka gani?

01/05/2026

🚨 RASMI: Burnley wametangaza kocha kuwa Scott Parker ameondoka katika klabu hiyo.

Michael Jackson atakuwa kocha wa muda hadi mwisho wa msimu.

fungua comment kuona picha nyingine ya kocha Michael Jackson.

30/04/2026

Mykhailo Mudryk amefungiwa miaka 4 na FA baada ya kushindwa kesi ya dawa za kulevya ya mwaka 2024. Nyota huyo wa Chelsea F.C. anatarajiwa kukata rufaa katika mahak**a ya usuluhishi wa michezo (CAS) .

Hebu angalia hii story kwa jicho la biashara ya mpira:
🔸 Alisajiliwa kwa €100M 💰
🔸 Akapewa mkataba wa miaka 7 (£100,000 kwa wiki)
🔸 Hajacheza kwa takribani miaka 2 😳
🔸 Sasa amefungiwa miaka 4 🚫
🔸 Na bado atabakiwa na mwaka 1 kwenye mkataba wake baada ya kifungo kuisha

Hii siyo tu hasara… ni project iliyofeli kabisa.

Je, huu ndiyo usajili mbaya zaidi kuwahi kutokea kwenye Premier League? 📉 🤔

30/04/2026

Anaitwa Mimisa Masato kutoka Kenya...
Ndiye alikuwa mwamuzi wa fainali ya Kombe la Muungano kati ya Simba SC vs Yanga SC.

Kwa ulivyomuona unampa asilimia ngapi?
Ana utofauti gani na Marefa wa Tanzania?

30/04/2026

MWENYE KITI WA BODI YA LIGI YA NBC ANAWEZA KUSEMA HIVI?

🚨🗣️ JAVIER TEBAS [Rais wa La Liga]:

“Barcelona inaweza kufikisha pointi 100 kwenye ligi? SIPENDI timu kufikisha pointi 100, ni nyingi sana.

Ni kweli kwamba Real Madrid na Atlético Madrid zimepoteza pointi nyingi na ziko chini ya kiwango chao cha kawaida, lakini sipendi bingwa kufika zaidi ya pointi 90.”

“Napenda ligi ambazo zinapata bingwa siku ya mwisho wa msimu.
Ndiyo maana ningependelea Barça isichukue ubingwa kwenye El Clásico.” 😂🤡

“Natumaini FC Barcelona hawatashinda ligi kwenye El Clásico wala kufikisha pointi 100.”

Sasa fikiria hali k**a hii ingetokea kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara… Mwenyekiti wa bodi ya ligi anasema wazi hataki bingwa awe na pointi nyingi au ashinde mapema 😅

Hapo ndipo ungeona presha ya mashabiki wa Young Africans, S.C., Simba S.C. na wengine ikipanda juu sana—wengine wakisema ligi inapangiwa matokeo, wengine wakisema ushindani unapotezwa makusudi.

Kwa kifupi, kauli k**a hizi zinaweza kuongeza drama na mjadala mkubwa kuliko hata matokeo yenyewe... 🔥

29/04/2026

Guillermo Ochoa ametangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Mexico baada ya Kombe la Dunia 2026.

Golikipa huyo pia anafikiria kustaafu soka mazima baada ya Kombe la Dunia.

27/04/2026

Mechi ya Derby ya Kariakoo kati ya Simba SC dhidi ya Yanga SC, Mei 03, 2026 kwenye uwanja wa MEJ. ISAMUYO itachezeshwa na Waamuzi kutoka Morocco 🇲🇦.

Hamza El Faruq - Refa wa Kati

Lahsene Azkawi - Msaidizi 01

Hamza El Nasri - Msaidizi 02

Mostafa Kchaaf - Fourth Official

27/04/2026

Gareth Bale 🗣️:

“Kama siyo majeraha, jina langu lingekuwa kwenye mjadala mmoja na Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.

Kwenye mazoezi ya Real Madrid, mimi ndiye nilikuwa bora kwenye mipira ya adhabu (free-kick), bora kwenye umaliziaji, lakini Cristiano alipendelea kupiga free-kick na mipira yote ya kutenga isipokuwa kona.
Ila kwenye mazoezi, asilimia yangu ya kufunga free-kick ilikuwa juu zaidi kuliko yake.

Dhidi ya Liverpool FC kwenye fainali, nilifunga bao la kipekee sana, lakini hakuna anayependa kukubali kwamba ndiyo bao bora zaidi katika historia ya UEFA Champions League kwa sababu tu jina langu ni Gareth Bale.”

Mwamba anatema ukweli mchungu...

27/04/2026

Jules Koundé alisema:
“Mchezaji wa mpira anaweza kukaa miezi sita au hata mwaka mzima bila kulipwa na bado akaishi maisha mazuri bila kuathirika kabisa.
Tofauti na watu wanaotoka nyumbani saa 1 asubuhi na kurudi saa 2 usiku, wakihangaika kupata kipato kidogo kwa ajili ya familia zao.

Sielewi kwa nini mashabiki wanawachukulia wachezaji wa mpira k**a mifano ya kuigwa. Siwapendekezi. Mfano halisi wa kuigwa ni baba anayefanya kazi kwa bidii kila siku kwa ajili ya familia yake.” 👏

Ukweli ni kwamba kauli hii inaumiza kidogo… lakini ina ukweli mkubwa sana ndani yake.
Tumefika mahali tunawajua wachezaji wa mpira kwa kila kitu—viatu wanavyovaa, magari wanayoendesha, maisha yao binafsi—lakini hatuwapi hata nusu ya heshima wale wanaopambana kila siku kuhakikisha familia zao zinaishi.

Kuna baba anatoka alfajiri, anarudi usiku, hakuna anayempigia makofi… lakini yeye ndiyo sababu familia ipo imesimama. Huyo hana spotlight, hana followers milioni… lakini ndiye role model wa kweli.
Sasa swali la kujiuliza ni hili—
Je, tunathamini watu sahihi au tumepoteza mwelekeo?

👇 Wewe unaonaje hii kauli?

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Kigoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Address


Osofia
Kigoma
ELKAKA