02/11/2021
JICHO MAKINI KWENYE 90 ZA YAΓGA SC NA RUVU SHOOTING.
Leo ilikuwa ni Mayele Vs Mohammed Makaka. Mashuti manne(4) ya Mayele yaliyo lenga lango yaliokolewa na Makaka Kwa ustadi mkubwa. Makaka ni miongoni mwa Magoli Kipa wazuri na wenye ubora sana kwenye hesabu.
Timu ilimmiss Khalid Aucho.Muunganiko na ushirikiano wa Yannick Bangala na Mukoko haukuwa kwenye Kiwango bora k**a ule wa Aucho na Mukoko. Aucho mara hucheza karibu sana kwenye pivot, Mukoko alicha nafasi kubwa kati yake na Bangala.
Djuma Shabani hakuwa na ufanisi Mkubwa leo hasa kabla ya kadi nyekundu ya Santos, Alipoteza pasi kadhaa. Niliamini baada ya Yanga kuongoza basi mabadiliko ya kumuingiza David Bryson yangekuwa kwa Djuma ili Kibwana aende kulia. Djuma anaonekana alitumia nishati kubwa kwenye Derby dhidi ya Azam FC.
Mkwasa alikuwa na mipango bora sana hasa kwenye alipo amua Kucheza kwenye falsafa ile ile ya umiliki wa mpira. Walifanikiwa kwa asilimia kadhaa walifanya play out from the back,walifanikiwa na build-up yao ilifia Katikati ya Uwanja. walikosa njia bora ama link-up Man kwenye kiungo na ushambuliaji.
Kadi nyekundu ya Santos Mazengo Ilibadili muelekeo kiuchezaji na mipango kiujumla (game approach) Kwa Ruvu Shooting. Baada ya kucheza kwenye total football na kurudi kufanya Low block huku wakitumia Counter Attack. Iliwarejesha Sana Yanga kwenye wepesi wa kuumiliki mchezo.
Emmanuel Mwandembwa ni miongoni mwa Waamuzi bora Nchi. Kadi nyekundu ilikuwa sahihi Kwa asilimia π― na, pigo la huru la penati lina maswali mengi sana hasa kwenye kuligundua k**a sio ama ndiyo. Ila Kwa namna ilivyo tokea basi Mwamuzi yeyote anaweza kutoa ama kutokutoa pia. Tukio tata.
30/10/2021
Yanga SC dhidi ya Azam FC Leo pale Kwa Mkapa. Ni Ligi Kuu NBC Tanzania Bara. Inaaminisha kwamba Yanga SC wanaingia k**a dominant than Azam FC kwenye huu mchezo. Ubora wa vikosi Vyote viwili utoa picha hiyo.
Azam na Yanga Kwa pamoja zinaoneka Kuwa na wachezaji individual wana uwezo, hawapishani Sana. Kuanzia kwenye ulinzi, Kiungo hadi Idara ya ushambuliaji. Japo Katika hili Yanga inaonekana Kuwa bora sana kwenye Kiungo.
Ubora wa Kiungo cha Yanga sio dhidi ya Azam FC tu, bali Kwa michezo hii kadhaa inaonesha wao ndo wenye Kiungo bora zaidi ya timu yeyeto kwenye NBC PL. Hii imewapa nguvu Nabi na Kaze Kuwa na timu yenye uwezo wa kucheza " Out from the back"
Aina ya uchezaji inayohitaji uwe na viungo bora kufanya ujenzi wa mashambulizi kutoka kwenye lao kwenda mbele Yani Kuwa viunganishi bora wa ulinzi na ushambuliaji kwa vertical direction possession. Nguvu nyingine ya Yanga ni Kwenye winga zao, Yacouba na Jesus Moloko.
Kwenye aina ya ujenzi wa mashambulizi ya Yanga wa Out play from the back, Job na Mwamunyeto na Aucho wamekuwa wazuri kwenye kutengeneza mashambulizi hollizontal kupitia Kwa Kibwana au Djuma na kuwawapa nguvu Sogne na Moloko.
Hivyo hivyo pia walifanya spread out vertical kupitia Kwa Bangala na Fei Toto akidaidiwa deep na Mayele wamekuwa wakifanya pressing kutoka Katikati au pembeni pia. Kinachowasaidi ni Kasi yao hasa dakika 45 za mwanzo.
Azam ili kuwazuia Yanga hasa Kipindi cha Kwanza ambacho wamekuwa bora sana, ni ku track back, kupitia Kwa iwe Zulu ama Nado, hasa upande wa Djuma amabaye anapanda Sana. Wakifanikiwa kuwazuia Yanga Kuanzia juua na kuwaondolea comfortability walinzi wao kuanza nyuma watafanikiwa kuwazuia.
Mkakati bora wa Kutengeneza mashambulizi baada kuzuia ni counter pressing kwenye Kasi ya Nado, anaoneka Yupo kweny top level ya Karia yake Kwa sasa. Anatengeza nafasi pia anafunga, uchezaji wake unawatengenezea space of playing wenzake kwenye mtirririko wa ushambuliaji.
Mchezo unamagoli siuoni kuisha Sare. Ni Chicken Man Vs Professor Nabi.
Robert Richard
27/10/2021
JICHO MAKINI KWENYE DAKIKA 90 ZA SIMBA SC NA POLISI TANZANIA.
Shukran Kwa Kocha Malale Hamsini wa Polisi Tanzania na Kocha Hetimana Thierry wa Simba SC, Kwa mchezo wenye hadhi ya Ligi Kuu, kiushindani,Kiufundi na Kimbinu. Ahsante Kwa wachezaji wote Kwa josho la ushindani kwenye dakika zote.
Hizi ni alama 3 muhimu zaidi Kwa Simba SC, kuliko pira biriani Yani soka la kuvutia Kwa wanamsimbazi. Siku zote timu inapojengwa hasa na Kuwa na mwalimu mpya basi ujenzi wenye kupata matokeo ndani yake huwa na mtirririko mzuri Kwa Mwalimu kufikia dhamira yake mapema.
Hetimana Leo alibadilika kwenye approach Mama ya Simba hasa kwenye kushambulia. Nguvu ya Simba kiushambuliaji huwa kutokea katikati. Hufanya high block kupitia namba 10, winga mara nyingi hufanya mikimbio ya kuingia ndani. Leo timu imefanya pressing kupitia pembeni hasa Kwa Dilunga.
Alipiga Krosi Kadha ambazo hazikutumika vema kutokana na uwepo wa idadi ndogo ya wachezaji wa Simba kwenye eneo la Polisi tofauti na Polisi mara zote walikuwa ni 4 Vs 1 yani walinzi wanne dhidi ya Kagere pekee. K**a Thierry anahamia kwenye pressing kupitia Wings atapaswa kutumia "double strike" watumie mipira ya Kros.
Larry Bwalya apunguziwe majukumu kichwani yanampoteze ufanisi. Aina ya wachezaji anaocheza nao kwenye kiungo wa hawachezi nae karibu kumpa box to box playing. K**a sio Kocha kumwambia,basi anaamini baada ya kuondoka Pacha wake Luis na Chama yeye ndiye Creator in Chief Kwa sasa.
Malale amefanya yote katika ubora mkubwa Ila ilifika wakati alihitaji kulazimisha wachezaji wake wa eneno la ushambuliaji wafanye pressing baada kufanikiwa kwenye Low block. Walikuwa compact kwenye kiungo na Ulinzi nyuma.
Unapofanikiwa kumzuia mpinzani kwa ufanisi ni unapaswa kutafuta magoli kwake. Polisi walikuwa na utulivu Mkubwa walipokuwa na mpira na bila mpira walizuia k**a timu. Tariq Seif, Adam Adam, Vitalis Mayanga na Daruweshi Saliboko walicheza taratibu sana jambo lilopelekea Simba kujipanga Kwa haraka kuzuia maeneo.
Endapo wangekuwa na Kasi na mgandamizo kuelekea kwenye box la Simba ingelazimisha makosa ya ulinzi Kwa Simba yaonekane.
Well done Mkongwe Yondan Kelvin. Polisi wana timu nzuri sana
27/10/2021
Timu 12 Kati ya 16 zilizo fuzu hatua ya makundi CAF champions League 2021/2022 zinafundishwa na Makocha Kutoka ndani ya Afrika.
Walid Regragui π²π¦-Wydad AC
Lassaad Chabbi πΉπ³-Raja Casablanca
Pitso Mosimane πΏπ¦ Al Ahly
Radhi Jaidi πΉπ³-EspΓ©rance de Tunis
Benni McCarthy πΏπ¦ - AmaZulu FC
Morena Ramareboli πΏπ¦- Galaxy FC
Nabil Kouki πΉπ³-ES SΓ©tif
Lassaad Dridi πΉπ³- Etoile du Sahel
Lamine N'Diaye πΈπ³- Horoya AC
Roque Sapiri π¦π΄- Sagrada Esparanca
Mateus Bodunha π¦π΄ - Petro AtlΓ©tico
Rhulani Mokwena πΏπ¦ - Mamelodi Sundown
NB. Mataifa ya Tunisia na Afrika Kusini Kwa pamoja wamekuwa na idadi ya makocha 4 kila Taifa. Jumla wamechangia makocha 8 kati ya 12 watokao Afrika. Angola inafutia Kuwa na Makocha 2 huku Morocco na Guinea yakiwa na Kocha mmoja mmoja.
26/10/2021
Kwa Mujibu wa ratiba hii ya michezo ya mtoanao hatua ya pili Shirikisho Barani Afrika, iliyotoka leo Oktoba 26/2021
Simba SC πΉπΏ itakutana na Red Arrows ya ZambiaπΏπ² mbali na Simba pia ratiba inaonesha Klabu nyingine Kutoka Tanzania Bara Biashara Utd,hatima yake bado ipo mikononi mwao. Mshindi kati yake na Al Ahli Tripoliπ±πΎ atakutana na Stade Malien ya Maliπ²π±
ngoma bado mbichi....
26/10/2021
IT IS OVER NA KAZI IENDELEE
Klabu ya Simba imetangaza kuachana na aliyekuwa Kocha wake Mkuu Mfaransa Didier Gomezi Da Rosa.
Kocha huyo alijiunga na Simba SC mwezi January 2021 ameitumukia Klabu hiyo Kwa miezi 10, amefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, FA CUP na kuifikisha timu hiyo robo fainali ya CAF Klabu Bingwa.
Mbali na Gomezi wengine walivunjiwa kandarasi ni Kocha wa viungo Adel Zrane πΉπ³ na Kocha wa Makipa Mbrazil Milton Nienov π§π·. Kwa sasa timu itabaki mikononi mwa Thierry Hetimana π·πΌ na msaaidizi wake atakuwa Selaman Matola πΉπΏ
Hatua hii imekuja siku chache baada ya Simba SC kutupwa nje ya Mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika Kwa msimu wa 2021/2022, na Jwaneng Galaxy ya Botswana π§πΌ
NB. Makocha wote Duniani huajiriwa Kwa makubaliano ama malengo mahususi. (Target) Kwa Simba SC misimu ya hivi karibuni wamekuwa na target ya kufika makundi hadi nusu fainali ya CAF champions league.
Makocha Kadhaa wamewafukuza Kwa kutokufikia lengo hilo Mama. K**a sio Kocha kufikia malengo miongoni mwa sababu nyingine ambayo hupelekea Klabu kumfukuza Kocha ni mwenendo mbovu, kiuchezaji, matokeo na mambo ya nje ya uwanja hasa nidhamu ya timu.
Je! Da Rosa alistahili kufukuzwa Kwa mujibu wa sababu tajwa hapo juu??
25/10/2021
TIMU 16 ZILIZOFUZU HATUA YA MAKUNDI TOTALCAFCL 2021/22
β’ Al Ahly πͺπ¬
β’ Zamalek πͺπ¬
β’ Etoile Sahel πΉπ³
β’ Sagrada π¦π΄
β’ Al Merreikh πΈπ©
β’ AmaZulu πΏπ¦
β’ Petro Atletico π¦π΄
β’ Raja CA π²π¦
β’ Mamelodi Sundowns πΏπ¦
β’ Jwaneng Galaxy π§πΌ
β’ Wydad AC π²π¦
β’ ES Tunis πΉπ³
β’ Horoya AC π¬π³
β’ Al Hilal Omdurman πΈπ©
β’ ES Setif π©πΏ
β’ CR Belouizdad π©πΏ
NOTE. Timu za Al Ahly Misri, Raja Casablanca, Wydad Casablanca na Esparance ST zenyewe zitaongoza Makundi baada ya Kuwa kwenye Pot 1. Michuano hii itawakilishwa na Kanda 4 pekee Kati ya 5 za CAF na 6 zilinazotambulika kimashindano ya CAF.
Ukanda wa Kusini COSAFA umeingiza timu 5 kwenye hatua hii kupitia timu mbili kutoka Afrika Kusini ambazo ni (AmaZulu na Mamelodi Sundown),timu mbil Kutoka Angola(Sagrada na Petro Atletico) moja Botswana (Jwaneng Galaxy)
Ukanda wa Mashariki na Kati CECAFA imeingiza timu mbili (2) zote zikitoka Taifa moja Yani Sudan ambazo ni El Merreikh na Al Hilal Omdurman.
Ukanda wa Magharibi yani WAFU ONE wao wameingiza timu moja pekee Horoya AC Kutoka Guinea .
Ukanda wa Kaskazin Yani UNAF, K**a ilivyo Kwa misimu mingine umekuwa kinara kwa kuingiza timu nyingi hatua ya makundi CAF champions League. Jumla ya timu 8. Wydad na Raja Casablanca kutoka Morocco.
Zingine ni Al Ahly na Zamaleck kutoka Misri, SR Belouizdad na ES Setif kutoka Algeria na Esparance ST,Etoile du Sahel kutoka Tunisia.
23/10/2021
CAF champions League 2021/2022. Timu ambazo zimefuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo hadi sasa.
Al Ahly πͺπ¬ β’
Zamalek πͺπ¬
Etoile Sahel πΉπ³
Sagrada π¦π΄
Al Merreikh πΈπ©
AmaZulu πΏπ¦
Petro Atletico π¦π΄
Raja Club Athletic π²π¦
Bado timu nane (8) zingine ili kulamilisha idadi ya timu 16
23/10/2021
Pichani ni Waamuzi wa uliopaswa Kuchezesha Mchezo wa Al Ahli Tripoli na Biashara Utd.
Uwepo wa Waamuzi Uwanjani tafsiri yake ni kwamba mchezo ulipaswa kuwepo. Kwa mantiki hiyo Waamuzi wameipatia matokeo ya ushindi Al Ahli Tripoli kikanuni, hii ni baada ya Biashara Utd kushindwa kufika Uwanjani.
Ikumbukwe Biashara imeshindwa kusafiri kuelekea Libya ikitajwa sababu za kiusafiri.
Mchezo wa awali iliopigwa Tanzania Biashara Utd ilishinda magoli 2 Kwa 0.
21/10/2021
TUZO ZA TFF VPL MSIMU WA 2020/2021
Golikipa bora Aishi Manula (Simba SC)
Beki bora Mohammed Hussein (Simba)
Kiungo Clatous Chama (Simba SC)
Mfungaji bora John Bocco (Simba SC)
Mchezaji Chipukizi Abdul Sopu (Coastal)
Mchezaji Muungwana Kibwana Shomari (Yanga SC)
Kocha bora- Didier Gomezi )Simba SC)
Mwamuzi bora Ramadan Kayoko(Dar Es salaam