Mokhan jr

Mokhan jr

Share

Football journalist Nimezalia Dar es salam

01/09/2026

Mchambuzi wa michezo wa Wasafi FM, Ricardo Momo, amesema mshambuliaji wa Simba SC, Libasse Gueye, anastahili zaidi kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Agosti. Momo amesema Gueye amekuwa na kiwango kizuri katika michezo yake ya mwanzo ya msimu, akionyesha mchango mkubwa kwenye kikosi cha Simba.

Hata hivyo, Momo amekiri kuwa Maxi Nzengeli naye anastahili kupewa nafasi katika mjadala huo kutokana na kiwango kizuri alichoonyesha katika michezo mitano aliyocheza. Pamoja na wote kuwa na kiwango kizuri, Momo anaona Gueye anastahili zaidi tuzo hiyo kutokana na mchango wake kwenye timu. Ricardo Momo amemuweka Gueye mbele ya Maxi Nzengeli katika mbio za Mchezaji Bora wa Agosti.

01/09/2026

WILSON ORUMA : YANGA SC MSHINDE KWA HALALI 🤔

“Yanga inabidi mshinde kwa halali, siyo kwa mipango mipango. Waamuzi wetu wachezeshe kwa haki,” amesema Oruma.

Huyu jamaa huwa anaichukuliaje Yanga SC ⁉️

01/09/2026

Top 5 ya wachezaji bora Agosti

1️⃣ — Libasse Gueye 📊 8.5
2️⃣ — Chadrack Boka 📊 8.3
3️⃣ — Max Nzengeli 📊 8.1
4️⃣ — Ismail Toure 📊 8.1
5️⃣ — Rushine De Reuck 📊 8.0

Kwa mujibu wa hizi rate za "SokaMetrics"
Libasse ndiye mchezaji bora wa mwezi wa 8.

01/09/2026

-Wengi watasifia pasi ya Aziz Ki kwenye bao la Shalulile na wengine watasifia muendelezo wa Shalulile kwenye upachikaji wa mabao...Ila kwangu mimi ile pasi ya Maxi Nzengeli kwa Aziz Ki ni ya kiwango cha juu sana...

Maxi na Mudathir ndio Yanga yenyewe sasa🔥

01/09/2026

Mchezaji wa Simba SC, Ibrahim Doumbia, amesema ameguswa sana na upendo na sapoti aliyopewa na mashabiki wa timu hiyo baada ya kushuka kwenye basi na kukutana na bango lenye ujumbe “WE ARE TOGETHER DOUMBIA. WE LOVE YOU.”

Doumbia amesema tukio hilo lilimgusa kiasi cha kumfanya kutokwa na machozi, akieleza kuwa katika soka kuna nyakati ngumu, ushindi, vipigo, lawama na wakati mwingine mashaka, lakini mashabiki wa Simba wamemkumbusha jambo moja muhimu kuwa hayuko peke yake.

Amesema mashabiki wote wa Simba tayari wana nafasi kubwa moyoni mwake na amewahakikishia kuwa ataendelea kufanya kazi kwa bidii, kupambana na kutoa kila alicho nacho kwa ajili ya jezi ya Simba.

“Nyakati hizi ngumu, In Shaa Allah, tutazishinda pamoja. Familia haitelekezi kila mmoja wakati wa changamoto. Familia hubaki pamoja, huinuka na kusonga mbele pamoja.”

Doumbia pia amewashukuru mashabiki wa Simba kutoka Tanzania nzima, wakiwemo wanaomhimiza, wanaomuombea, wanaomuamini pamoja na wanaomkosoa, akisema anawapenda wote na maoni yao yanampa nguvu zaidi ya kufanya kazi kwa bidii na kuwa bora.

Amesema hataki kuzungumza sana, bali anataka kufanya kazi, kujifunza, kuboresha uwezo wake, kupambana na muhimu zaidi kulipa upendo wa mashabiki kwa kiwango kizuri uwanjani.

“Nyakati bora bado zinakuja, In Shaa Allah. Asanteni kwa kila kitu, familia yangu ya Simba. Asanteni kwa upendo wenu, uvumilivu wenu na sapoti yenu. NAWAPENDA NYOTE. Simba Nguvu Moja!”

31/08/2026

Unadhani mchezaji gani anashahili tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa nane Kati ya libasse Gueye na Maxi Nzengeli?

Ikiwa Libasse Gueye ana goli 1 na assist 5 katika mechi 5 na kufanikiwa kubeba tu 2 za mchezaji bora katika mwezi huu.

Maxi Nzengeli akiwa na mabao 3 na hana Assist katika michezo mitano huku akikusanya jumla ya tuzo 5 za man of the match kwenye mwezi huu wa nane.

Je, kwa mtazamo wako Nani anastahili tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa nane??

31/08/2026

Umri wake unaweza kuwa mdogo sana ila Jezi aliyovaa ni nzito sana, Mchezaji mzuri ila akomae zaidi na basics kwasasa wala asihangaike kudhihirisha chochote aambiwe tu aingie Uwanjani kufanya vitu sahihi na magoli yatakuja, asijipe presha Bwana Mdogo maana hakuna aliyemwekea timu mabegani acheze tu mpira wa miguu.

31/08/2026

Kiungo mshambuliaji mahiri Feisal Salum 'Feitoto' ameanza kazi rasmi ndani ya Ligi Kuu ya NBC kwa kishindo baada ya kuwafunga Kagera Sugar na kuiongoza Azam FC kuibuka na ushindi safi wa mabao 2-0 ugenini. Uwepo wake kikosini unaendelea kuongeza ufanisi mkubwa na kuipa nguvu timu hiyo.

31/08/2026

Alama tatu muhimu kwa Mnyama, Simba SC katika dimba la Meja Janerali Isamuhyo kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi ya Geita Gold FC kwenye mchezo wa mzunguko wa tano wakifikisha alama 15 baada ya mechi tano huku wakiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.

Nyota wa mchezo huo, Libasse Gueye amefunga bao lake la kwanza kwenye Ligi kuu bara mpaka sasa na kutoa asisti moja ikiwa ni jumla ya mchango wa magoli sita kwenye mechi tano za ligi, bao moja na asisti tano

Nathaniel Chilambo ameendelea kumpa Mwalimu Steve Barker machaguo zaidi, unamkuta kwenye maeneo matatu na anafanya kazi ile ile, beki wa kushoto, kiungo wa kati na winga, mpe chafu anakupa safi na amemaliza mechi na asisti.

31/08/2026

🚨 JUST IN — MASWALI MAZITO JANGWANI!

Kuna taarifa zinazozagaa kwamba Yanga SC inaweza kukumbana na adhabu ya kupokwa pointi 3 kutokana na suala la usajili wa Selemani Mwalimu “Gomez” na kushiriki kwake dhidi ya Pamba Jiji.

K**a taarifa hii itathibitishwa rasmi, basi hili si jambo dogo hata kidogo. Kanuni za usajili zipo kwa ajili ya kila klabu—mchezaji ambaye hajakamilisha taratibu zinazotakiwa hastahili kushushwa uwanjani mpaka awe eligible.

Na hapa ndipo tunataka majibu ya wazi:

Gomez alikuwa amesajiliwa na alikuwa eligible kucheza siku hiyo, au kulikuwa na taratibu ambazo bado hazijakamilika?

Kwa sababu k**a kweli kulikuwa na ukiukwaji, basi zile pointi tatu mlizoshangilia uwanjani zinaweza kugeuka kuwa pointi tatu za mezani kwa mpinzani.

Lakini tusikimbilie kusherehekea au kuhukumu kabla ya barua rasmi kutoka TFF/TPLB. Mpira una kanuni, na kanuni hazijali ukubwa wa klabu.

Jangwani, safari hii barua ndiyo itakayocheza dakika 90. 😏🔥🟢🟡

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Mkuranga?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address


Mbezi
Mkuranga