YANGA Sports Updates

YANGA Sports Updates

Share

We offer you a daily sports news

06/04/2026

Achana na porojo za walioshindwa.. Simba timu yao ni mbovu sana, wanapo shindwa kutimiza walicho tegemea huja na vimakosa vya kijinga.. Leo hii kilicho waangusha ni wachezaji hao hasa Geye na Mwenzake Aura.. Jamaa ni wachoyo sana, Wana mambo mengi ambayo kimpira hasa mechi ngumu hutakiwi kufanya. Kila mmoja anataka kuonyesha kuwa yeye ni fundi wa boli, hawako tayari kucheza kimkakati ili kuisaidia timu.

Mashabiki kazi yao ni kuja kulialia bila kuangalia majukumu ya hovyo wanayo fanya wachezaji wao.
Binafsi lawama anazopewa refa ni kutafuta kichaka cha kujificha kwa ubovu wa timu yenu.. Na nivile mmekutana Azam naye kiazi kwa sababu nafasi k**a ile ya Sadun unakosaje kufunga? Yote tisa.. Kumi. Arajiga ni tunu ya Taifa kwa marefa hapa Tanzania.. Anatakiwa kulindwa, k**a binadamu anamakosa yake lakini kwa leo amechezesha vizuri bila wasi Wasi wowote.
Mkianza milio ya marefa itakuwa ni dalili ya kushindwa coz badala mjikite kutengeneza timu, nyie mko bize kutaka ubingwa wa Email.

25/10/2025

Karibu Jangwani, Kocha wa Sayansi ya Mpira Pedro Gonçalves🔰

Taarifa zaidi tembelela Yanga SC APP📲


25/10/2025

🚨🚨 DEAL DONE: Yanga wamemuajiri kocha wa zamani wa Ekenäs ya Finland,Casa Pia ya Ureno,na timu za vijana za Sporting Lisbon,Filipe Duarte da Silva Pedro,kuwa kocha msaidizi wa timu hiyo✅

Kocha huyo ataambatana na kocha mkuu Pedro Gonçalves ili kuinoa Yanga.

Ikumbukwe walikuwa pamoja kwenye timu ya taifa ya Angola.

Balaa jingine limetua NBC😄 na pia Young Africans Sports Club imemuajiri kocha msaidizi

Yanga wamemuajiri kocha wa zamani wa Ekenäs ya Finland,Casa Pia ya Ureno,na timu za vijana za Sporting Lisbon,Filipe Duarte da Silva Pedro,kuwa kocha msaidizi wa timu hiyo✅

Kocha huyo ataambatana na kocha mkuu Pedro Gonçalves ili kuinoa Yanga.

Ikumbukwe walikuwa pamoja kwenye timu ya taifa ya Angola.

Kwa habari za Yanga follow Shabani Fundi Sport kwa update za mechi za Yanga na zote kwa ujumla


SHABANI FUNDI SPORTS

19/10/2025

"BREAKING: Miongoni mwa majina ambayo yanajadiliwa na Yanga ili kuchukua mikoba ya Romain Folz ni kocha Mreno, João Paulo Mota Maria.

Yanga wako Tayari kuvunja mkataba wake Huko Oman na kumleta Jangwani."

follow 👉 me

19/10/2025

Jina la kocha wa kimataifa kutoka nchini Ureno João Paulo Mota Maria lipo kwenye orodha ya makocha ambao klabu ya Young Africans inawatupia macho.

Mara baada ya Klabu ya Young Africans kumtimua aliyekuwa kocha wao mkuu Roman Folz, sasa wako sokoni kusaka kocha mkuu mwingine.

Kocha huyu anauzoefu na soka la Afrika kwani amevifundisha vilabu baadhi ikiwemo klabu ya soka ya Al hilal Omdurman na timu ya taifa la Sudan.

18/10/2025

TAARIFA KWA UMMA


11/10/2025

Viwanjani ⚽ 📸: Uongozi wa klab ya Young Africans Ulipitia kwanza CV za kocha Romuald Rakotondrabe na kujiridhisha kuwa anastahili Kuwa Kocha Mkuu wa klab yao ndipo walipoanza mazungumzo na kisha kukubaliana nae kila kitu,

Pia Uongozi wa klab ukahitaji kupitia na CV za wasaidizi wake na kisha kubaini Kocha msaidizi namba moja hana vigezo, Hana leseni B ya CAF hivyo Uongozi wa klab Umemtaarifu Roro kutafuta msaidizi mwenye vigezo Kamilifu,

Kocha Roro ameutaarifu Uongozi kuwa kwasasa hawezi kutafuta msaidizi mwingine na hayupo tayari kuanza safari ya kuja Tanzania kufanya kazi bila msaidizi wake huyo,

Hivyo Uongozi wa klab ya Yanga unatarajia kuangalia ingizo lingine la Kocha Mkuu Mpya na kuachana na kocha huyo aliyefanya vyema kwenye Mashindano ya Chan akiwa na Taifa la Madagascar,

Means dili la Roro kuja Young Africans lina ugumu na muda wowote Young Africans wanabadili gia angani 🙌

02/05/2025

ANAANDIKA JAMES TUPATUPA, Mchambuzi CLOUDS.


Je bado nguvu ni moja au nguvu sasa ni nyingi, kuna namna waamuzi wetu wanapewa nguvu ya ziada na wanahakikishiwa kubaki kazini no matter what, ndio maana wanafanya wanayofanya.
.
Kiukweli soka letu lina mipango mingi sana, ndio maana kuna watu ukiwaambia ligi yetu ni namba sita sijui tano kwa ubora Afrika wanakuona mlevi wa gongo tu, kila kitu kinapangwa nyuma.
.
Kuna watu wameweka hela kwenye timu zao wanalia machozi ya damu, KenGold unaambiwa katia takriban 1.5B akitegemea fair competion, kilichomkuta mmekiona wote.
.
Timu ndogo ambazo sio sehemu ya mipango ya timu kubwa zinalia balaa, nguvu, muda, na hela vimepotea kwa pamoja, kuna wakati itafika kutakua na ligi tatu, ligi ya Simba Yanga na Azam, kisha ligi ya timu zinazobaki ukitoa Simba Yanga na Azam, halafu ligi ya muungano inayoshirikisha Simba Yanga Azam na timu zinazobakia.

24/04/2025

KUNA WAKATI MAISHA YA MPIRA YANATUPA HUZUNI SANA 🔰🔰🔰

Ameandika PriPrince DeogratiusMchambuzi wa soka sports

Hakuna wakati mgumu sana kwenye mpira k**a ule wakati ambao mchezaji pendwa anaondoka kwenye timu,

Huu huwa wakati mgumu sana kwa mashabiki hususani wale wanaotambua mchango wa huyo mchezaji,

Huu ni wakati mwingine kwa wananchi yanga sc kumkosa mchezaji wao pendwa Master Ki

Aziz Ki anaondoka yanga sc mwisho wa msimu huu hivyo huu ni msimu wake wa mwisho akiwa na jezi ya yanga sc,

Actually zimebakia mechi 6 tu kumuona Aziz Ki uwanjani akiipigania yanga sc,

Binafsi nitamkumbuka sana kwa jitihada zake ndani ya yanga sc,
Pia mchango wake ndani ya yanga sc,

Kwenye misimu aliocheza hapa bongo kuna mafanikio makubwa sana kachangia ndani ya yanga sc,

Sijui ni nani ataziba nafasi yake.... Lakini maisha lazima ya endelee mbele,

Nilitamani kuendelea kumuona Aziz Yanga SC lakini na yeye pia ana ndoto zake kwenye maisha ya soka,

Kila la kheri mwamba Stephane Aziz Ki, ukafanikiwe pia huko uendako lakini Tanzania tunakupenda sana na tulifurahia sana kuwa na wewe kwenye kila nyakati tulizopotia kwa pamoja,

Hamasa yako uwanjani kwa wachezaji wenzio na wachezaji pinzani tutaikumbuka milele

Hakika umeacha alama kubwa sana kwenye mioyo ya wana Yanga SC,

Good bye Aziz Ki 💛💚💛💚

sports

22/04/2025

SIMBA SIO TISHIO

🗣️”Tutabadilisha matokeo sio lazima kushinda 2-0,Tunaweza kushinda 1-0 na kwenda kwenye mikwaju ya penati”

“Simba SC sio tishio kwa kile nilichoona wanafungika na njia ya fainali bado ipo wazi”

-STEVE BARKER,Kocha mkuu Stellenbosch FC

Nene Yanga Fans HQ

21/04/2025

KILELENI JOTO LIMEPUNGUA KWA 13°C

Naelewa kwanini Fountain Gate FC walicheza mipira mirefu kwenda kwenye box la Yanga SC kabla ya kuruhusu goli;

1. Yanga SC hatari sana kutengeneza na kutumia nafasi finyu.
2. Tusiondoke kwetu tudumisha umbo la kiulinzi kwa idadi nzuri ya wachezaji.
3. Tunataka tukabe mtu-na-mtu leo hawatoki.

Ukitumia mipira mirefu kushambulia hakikisha vitu hivi: mnashinda second-balls zote+ufanisi mzuri kwenye mapambano ya mwili (msicheze madhambi)+utimamu wa mwili upande wenu uwe-juu kwajiri ya kufanya: Counter pressings na kupora mipira

✅.Goli zote mbili walizofungwa Fountain Gate FC ni makosa binafsi ya John Noble (GK) unawezaje;

_kutema mpira kirahisi vile mbele ya Mzize ndani ya box lako.
_GK wa daraja lake umepokea mpira nje kabisa unauleta vile kwenye box lako.? ile ni zawadi ya Psaka kwa Azizi Ki.

Fountain gate fc walitupa sana mipira, Yanga SC muundo wao ukawa 2:2:3:1:2 'position rotations' za wachezaji wakaifanya ikawa tofauti kila dakika na kumiliki mpira walivyotaka.

Yanga SC no pressure kwenye eneo lao Diara(GK) ongezeka kwa Bacca+Job kuanza 'buildup' inasaidia double pivot Yao (Duke+Mudathiri) kufanya runs za kupokea mipira wakati Aziz Ki+Nzengeli wanasoge nchini na kuvuruga kabisa ulinzi wa Fountain.

_ikatoa nafasi kwa Mwenda+Kibabage kwenda pembeni sana kupiga krosi au V-passes Kwajiri ya Dube+Mzize kwenye box la mpinzani, ilikua hivi kwenye goli lao la tatu la Yanga SC.

Kwanini Yanga SC hawapati tabu kwenye kukaba.? Kwa sababu;
_wanatumia 2+3/2+1 rest-defence system: idadi nzuri wakati wa kujilinda kwenye turnovers au transitions, bila shida sana.

_Yanga SC wanafanya gengen pressings mda wote: wanajua wapinzani wengi kwenye ligi sio bora kutumia transitions, tutakaba hapo hapo mpira ulipopotea.

Goli la nne kwa Yanga SC limetokana na ikabu ilikua miss-position ya Parapanda (GK)+ukuta kushindwa kuruka kwa nguvu, kwa ubora wa Chama utadhibiwa tu, ni quality ilioko kwenye kikosi chao kumbuka alipishwa na Aziz Ki.

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Morogoro?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Website

Address


342 KIDATU
Morogoro