07/02/2025
*SEMINA KWA WAKULIMA NA WAFUGAJI*
Juzi jumatano tarehe 5/02/2025 timu ya wataalamu kutoka Mrutu Agro-Solutions Co.Ltd (MAS), ambao ni Philipo Mrutu, Yusuf Juma na Robert Jonathan walitoa semina kwa wakulima na wafugaji wa Kijiji cha Naberera, Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara. MAS pamoja na mambo mengine, tunasaidia wakulima, wafugaji na wadau wengine kwenye mnyororo wa thamani kupitia mafunzo mbalimbali ya muda mfupi ili kuwajengea uwezo na kuwapa suluhisho makini kwenye changamoto mbalimbali.
Daktari wa mifugo Dkt. Juma Yusuf aliwapa elimu na mbinu za Ufugaji kibiashara na msisitizo mkubwa ulikuwa kwenye kuzingatia kanuni za ufugaji wenye tija ikiwa ni pamoja na biashara ya kunenepesha mifugo, ufugaji wa ng'ombe wa kisasa wa maziwa na kuanzisha mashamba ya majani ya malisho.
Mtaalamu wa kilimo cha ufugaji wa samaki Bw. Robert Jonathan alitoa elimu na hamasa ya ufugaji wa samaki akisema kuwa binadamu hutegemea kupata takribani 40% ya protini kutokana na samaki, vyanzo vya asili havitoshelezi mahitaji na mahitaji yanazidi kuongezeka kadiri idadi ya watu inavyozidi kuongezeka hivyo ufugaji wa samaki ni fursa nzuri ya biashara inayoweza kuwaingizia watu kipato.
Mkurugenzi wa MAS ndugu Philipo Mrutu ambaye pia ni mtaalamu wa sayansi ya Uchumi Kilimo na Kilimo Biashara alielezea jinsi ambavyo kampuni imejipanga kuwahudumia wadau mbalimbali ikiwemo wakulima na wafugaji kutokana na mahitaji yao waliopo vijijini na hata wa mijini ndio maana wamefika baada ya mwaliko huo kupitia mwenyekiti wa Chama cha Mazingira na Ufugaji Tija Tanzania (CHAMAUTA) Mkoa wa Manyara ndugu Naftal Samweli. Washiriki wa mkutano pia walielimishwa juu ya umuhimu wa kutunza kumbukumbu, mbinu za kuongeza thamani na Tija, maandiko ya miradi na fursa za mitaji kutoka taasisi mbalimbali za kifedha nchini na elimu ya ujasiriamali.
Kwa mahitaji ya semina na mafunzo ya muda mfupi, huduma na bidhaa mbalimbali kuwezesha kufuga na kulima kibiashara wakulima, wafugaji na wadau mbalimbali wanakaribishwa kushirikiana katika kusaidia kuleta mabadiliko chanya na maendeleo kupitia fursa mbalimbali zinazo tuzunguka.
Sambamba na hayo, kampuni ya MAS inatoa huduma na bidhaa mbalimbali ili kusaidia wakulima na wafugaji kuongeza tija kwenye shughuli zao, kupunguza gharama, kuwaunganisha na fursa za masoko ya ndani na nje ya Tanzania, kuwaunganisha na taasisi za kifedha kupata mitaji kuongeza faida na kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi k**a ifuatavyo:-
✍️Upatikanaji wa Miche bora ya matunda, miti, kivuli, mbao, maua, mbegu ya Majani ya mifugo k**a vile Neppier, Molato, n.k ( _Seedlings production & Supply_ )
✍️Kuwatembelea wadau na kutoa ushauri wa kitaalamu ( _farm visiting, farm planning, farm layout, farm design, Agro consultancy, ect_ )
✍️Kupimiwa udongo kwenye shamba lako ( _soil testing &analysis_ )
✍️Ujenzi wa mifumo ya umwagiliaji shambani mwako ( _installation of Irrigation system ie. Sprinklers, drip irrigation system ect_ )
✍️Ujenzi wa vitalu nyumba ( _installation of greenhouse and solar dryers_ )
✍️Ujenzi wa mabanda ya mifugo k**a ng'ombe, mbuzi, kuku, kondoo, nguruwe, n.k.( _Construction activities_ )
✍️Huduma ya kupandiwa miche shambani, _planting, prunning,_ n.k.
✍️Kuandikiwa mpango wa biashara ( _andiko la mradi ili kupata mkopo kwenye taasisi za kifedha au kwa matumizi mengine k**a ufadhili au kupata wadau / wabia wa Biashara na Uwekezaji_ )
✍️Mafunzo ya kujiandaa kustaafu ( _Kwa walio ajiriwa namna ya kujiandaa kustaafu na tunawapa huduma endelevu_ )
✍️Mafunzo ya kilimo biashara na ujasiriamali kwa vikundi, taasisi, vijana, wanawake, wanaume, n.k.
✍️Kuanzisha mashamba darasa kwenye shule za msingi, sekondari, vyuo n.k
✍️Huduma ya usimamizi wa miradi ya kilimo, Ufugaji n.k ( _Upatikanaji wa vijana wa SHAMBA au Usimamizi Kimkataba_ )
✍️Huduma ya Ujenzi wa mabwawa ya samaki, na huduma zingine zote k**a vifaranga wa samaki, chakula, ushauri, masoko n.k.
✍️Kufanya Kilimo cha Mkataba Kibiashara
✍️Upatikanaji wa mashamba n.k
✍️Huduma zingine zinazo endana na kilimo biashara, Ufugaji, Uvuvi na Ujasiriamali k**a vile uchimbaji wa visima virefu n.k.
✍️ Upatikanaji wa mbegu Bora za Ufugaji wa Ng'ombe, Nguruwe, Kuku, Kondoo, Bata, Kanga n.k
✍️ Huduma ya masoko ya bidhaa na mazao yatokanayo na Kilimo Mazao, Mifugo, Uvuvi na Misitu
✍️Huduma ya kupima shamba na kupata hati miliki
✍️ Huduma saidizi za Kilimo Biashara kutokana na mahitaji ya mteja k**a vile usaidizi wa kusajili kampuni, jina la biashara, NGOs, n.k.
✍️Usambazaji wa Mitambo mbalimbali, Mashine na Pembejeo zote za Kilimo na Mifugo ikiwemo Trekta, Planter, mbegu, viuatilifu na mazao /bidhaa za kilimo na Mifugo, n.k
✍️ Huduma na shughuli za Ukandarasi, ubunifu, usimamizi na utekelezaji wa miradi ya Kilimo na Ufugaji.
*_"Suluhisho makini kwa Uwekezaji Katika Kilimo Biashara, Ufugaji bora, Uvuvi na Ujasiriamali kwa Maendeleo Endelevu"_*
*Mrutu Agro-Solutions Co. Ltd*,
Simu: *0753442903📞*
Email: *mrutu.agrosolutions .com*
Angalia Catalog hapa👇👇👇
https://wa.me/c/255753442903;
Website: www.mrutuagrosolutions.co.tz