20/07/2020
TETESI ZA SOKA MICHEZONI LEO JUMATATU.
Winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, 20, huenda akahitajika kuanzisha mwenyewe hatua ya kutaka kuhamia Manchester United kwa kusema wazi kwamba anataka kuondoka klabu ya Ujerumani. (Mirror)
Juventus inachochea hamasa ya timu zinazomtaka mshambuliaji wa Brazil Douglas Costa, 29, katika ya Manchester City na Paris St-Germain na wanataka nafasi yake ichukuliwe na mshambuliaji wa Wolves na Mexico Raul Jimenez, 29. (Tuttosport)
Kiungo wa kati wa Arsenal raia wa Uhispania Dani Ceballos, 23, yuko tayari kumuomba rais wa Real Madrid Florentino Perez aongeze makubaliano yake ya mkopo na Gunners kwa msimu mwingine. (El Confidencial, via Express)
Leeds United ambayo ndio ya hivi karibuni kupandishwa daraja imethibitisha kwamba winga mwingereza wa Manchester City, Jack Harrison, 23, atasalia kwenye klabu hiyo kwa makubaliano ya mkopo kwa msimu mwingine. (Manchester Evening News)
Kiungo wa kati wa West Ham,16, Benicio Baker-Boaitey amepangiwa kujiunga na Bayern Munich na atasafiri hadi Ujerumani kwa mazungumzo, baada ya kukataa ombi la kusaini mkataba wa makubaliano ya mchezaji wa kulipwa na Hammers atakapokuwa anatimiza miaka 17 Januari. (Sun)
Kiungo wa kati wa Brazil Willian, 31, anayehusishwa na Tottenham, Arsenal na Manchester United - amefichua kwamba ni miongoni mwa watakaocheza mechi inayosubisiriwa ya Chelsea kwa mkataba mpya baada ya kuomba makubaliano ya miaka mitatu na akapewa miwili. (De Sola, via Mirror)
Kocha wa Newcastle Steve Bruce anahofia kwamba bajeti yake ya msimu ujao itapunguzwa kwasababu mapato ya klabu hiyo ya pauni milioni 170 mwaka jana yatapungua kutokana na kupungua kwa malipo ya matangazo na kurejeshewa mashabiki pesa zao walizokuwa wamelipia tiketi za mechi msimu huo. (Mirror)
Kuimarika kwa mchezo wa mlinzi wa Brazil David Luiz, 33, huenda kukabadilisha mawazo ya Mikel Arteta wakati kocha huyo wa Arsenal anajitayarisha katika dirisha la usajili msimu huu. (Star)
Manchester United ilimpa Jude Bellingham na wazazi wake fursa ya kutembelea eneo la kufanyia mazoezi, huku Sir Alex Ferguson akiwepo, katika jaribio la kumshawishi kiungo huyo wa kati wa Birmingham, kufikia nao makubaliano lakini badala yake akachagua kwenda Borussia Dortmund. (Mail)
Ushawishi wa Tottenham kwa kiungo wa Southampton Pierre-Emile Hojbjerg, 24, umesababisha hali ya wasiwasi kuhusu mustakabali wa kiungo wa kati Harry Winks,24, katika klabu hiyo. (Sunday Mirror)
Wakati huo huo Hojbjerg amemwambia kocha Ralph Hasenhuttl kuwa hataongeza mkataba mpya na klabu hiyo(mirror)
Mshambuliaji wa Manchester United Mason Greenwood, 18, atapata dili mpya Old Trafford kiasi cha pauni 40,000 kwa wiki ikiwa ni miezi tisa tangu kusaini mkataba wake. (Sun on Sunday)
Kocha msaidizi wa Aston Villa John Terry anafikiriwa na Bristol City kuwa kocha wao ajaye baada ya chaguo lao la kwanza Steven Gerrard kukataa kuhamia katika klabu hiyo. (Sunday Express)
Borussia Dortmund inataka dau la pauni milioni 115 kumuachia Jadon Sancho, lakini mchezaji huyo wa nafasi ya mshambuliaji anayehusishwa na taarifa za kuhamia Manchester United, amekataa kuondoka kwenye klabu hiyo ya Ujerumani (Sunday Express)
Manchester City wako kwenye mazungumzo na Gremio kuhusu dili la pauni milioni 4.5 kwa ajili ya kiungo wa kati Diego Rosa,17. (Mail on Sunday)
Mshambuliaji wa Manchester United Mason Greenwood, 18, atapata dili mpya Old Trafford kiasi cha pauni 40,000 kwa wiki ikiwa ni miezi tisa tangu kusaini mkataba wake. (Sun on Sunday)
Arsenal wako tayari kufikia dau la oauni milioni 40 kwa ajili ya mshambuliaji wa U17 Joelson Fernandes,17, anayekipiga Sporting Lisbon ambaye pia anazivutia Barcelona na Juventus (A Bola-in Portuguese)
Kocha wa Sheffield United Chriss Wilder amesema kuwa usajili wa mlinda mlango Wes Foderingham,29, hauna maana kuwa Dean Henderson ataondoka katika klabu hiyo na kuonesha matumaini kuwa mchezaji huyo,23, atasalia akichezea kwa mkopo kutoka Manchester United katika msimu mwingine. (Maii Sunday)
Mkurugenzi Mtendaji wa Leeds Angus Kinnear amesema kuwa wamiliki wa klabu watakutana na kocha Marcelo Bielsa juma lijalo kujadili kuhusu mkataba mpya na kufanyia kazi malengo ya usajili wakati wanaporejea ligi ya primia msimu ujao. (Sunday Express)
Zenit St Petersberg wako tayari kutoa ofay a pauni milioni 9 kwa ajili ya mchezaji wa nafasi ya ulinzi Dejan Lovren,31, lakini mabingwa hao huenda wakahitaji kitita cha takribani pauni milioni 15 kwa ajili ya mchezaji huyo, raia wa Croetia. (Mail on Sunday)
Villarreal imethibitisha kuwa Santi Cazorla amechagua kutoongeza mkataba na klabu hiyo, wakati kukiwa na tetesi kuwa kiungo huyo wa kati ,35, anaweza kurejea Arsenal. (Sunday Mirror)
Kiungo wa kati wa QPR Bright Osayi-Samuel,22, anajiandaa kufanya vipimo katika klabu Bruges baada ya vilabu kukubaliana ada ya pauni milioni4.75. (Mail on Sunday)
Kocha wa Everton Carlo Ancelotti anaamini kuwa ataungwa mkono na bodi ya klabu katika kipindi cha dirisha la usajili baada ya kusema kuwa kikosi chake kinahitaji maboresho. (Sky Sports)
Mlinzi wa kushoto wa simba Gadiel Michael k**agi amekanusha tetesi za kuwa yuko karibuni kurudi yanga baada ya kukosa nafasi ya kudumu akisema hizo ni kelele za chura tu ............!
Kona ya vijineno "Kila ninapokwenda kwenye tuzo kubwa duniani zinazonikutanisha na Lionel Messi mwanangu Ronaldo Jr. lazima aende akasalimiane na kushikana mikono na messi huwa anapenda sana kumuangalia uwanjani ndiyo maana inapotekea nafasi ya kuonana naye huwa hapotezi hata dakika moja that is football - Christian Ronaldo"
20/07/2020