21/12/2023
Embu tupige picha ya pamoja au embu kaeni hapo niwapige picha ni miongoni mwa kauli zinazotumika kabla mtu au watu hawajaamua kupiga picha.
Hii ilikua mwaka 2016 wakati tukiwa Star Tv na rafiki zangu na ,miaka imepita,siku zimepita mno lakini tunamshukuru Mungu bado tuko hai.
Mpangilio wa Picha kutoka kushoto ni Dickson,Peter, Hope,usichanganywe na wingi wa nywele nlizokuwa nazo😂
08/12/2023
Huku yalikotokea majanga maporomoko ya udongo ni makao makuu ya wilaya yetu ya Hanang' yaani mji wa Qatesh tunakoishi sisi kunaitwa Endasaki umbali wa kilomita zaidi ya 20 kutoka Qatesh mjini,poleni sana ndugu jamaa na marafiki kwa janga hili zito,Mwenyezi Mungu awape faraja katika kipindi hiki kigumu.
25/11/2023
Kila la kheri Mnyama,wengine naskia lolote tayari limewakuta
14/10/2023
Uendelee kupumzika kwa amani Hayati J.K.Nyerere
23/01/2020
MKUU WA JESHI LA ZIMAMOTO APIGWA CHINI:Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemuondoa kwenye nafasi yake Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, Thobias Andengenye kutokana na kuidhinisha mradi wa zaidi ya Trilioni 1 ambao haujapitishwa na bunge.
23/01/2020
Rais John Magufuli amesema Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Meja Jenerali Jacob Kingu ameandika barua ya kujiuzulu na amemkubalia
23/01/2020
BREAKING NEWS : WAZIRI WA MAMBO YA NDANI AJIUZULU
Rais Magufuli amethibitisha kuwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola amejiuzulu nafasi yake.
"Ninajua Waziri wa Mambo ya Ndani hayupo hapa ameshaandika barua ya kujiuzulu na mimi nimeshamkubalia" - Rais Magufuli
10/01/2020
Ratiba ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) mzunguko wa 4.