Mwanza Ndiyo Home-MNH News

Mwanza Ndiyo Home-MNH News

Share

1.0) JINA LA CHAMA

i. Jina la chama ni MNH

ii. Kirefu chake ni " MWANZA NDIYO HOME"



2.0) IMANI ZA WANA MWANZA NDIYO HOME

i. ii. iv. v. iii. vi. Misiba

ii. vii.

Wana MNH wote ni kitu kimoja katika shida na raha. Wana MNH ni lazima tukuze mfuko wetu wa chama. iii, Vilevile tunaamini kwamba mti mmoja haujengi nyumba na kidole kimoja hakivunji chawa. Wanachama wote ni sawa bila kujali umri,hadhi au uongozi. Fitina,majungu na upendeleo ni mwiko kwetu.



3.0) DHUMUNI/ DIRA

i. Kumfariji mwanachama aliyepatwa na msiba au tatizo lolote. Kuwa sambamba naye kwa

Photos 14/01/2019

Baada ya kushusha kipigo kwa Waarabu, Mabingwa wa soka Tanzania, Simba SC Jumamosi hii watakuwa ugenini Kinshasa DRC kukipiga na AS Vita Club, katika mechi ya kundi D Ligi ya Mabingwa Africa.

Utashuhudia Live mchezo huu kupitia ZBC2, kuanzia saa moja kamili Usiku.

Photos 13/01/2019

Full time: La liga

Athletic Bilbao 2-0 Sevilla
Goals: Williams 23' 84'

Photos 13/01/2019

Mtoto wa Rais Trump atajwa kugombea nafasi ya urais wa Benki ya Dunia

Imefahamika kwamba Ivanka Trump binti wa rais wa Marekani, Donald Trump,ni moja ya majina yanayotajwa kuwania nafasi ya rais ya benki ya dunia (WB).

Gazeti la Financial Times limeripoti kwamba baada ya rais wa benki ya dunia Jim Yong Kim, kujiudhuru kazi hiyo. Katika watu wanaotajwa kuitaka nafasi hiyo ni pamoja na binti wa rais wa Marekani Ivanka Trump, pamoja na balozi wa kudumu wa Marekani katika umoja wa mataifa aliyemaliza muda wake Nikki Haley. wengine ni pamoja na rais wa wakala wa maendeleo wa Marekani Mark Green pamoja na mshauri wa masuala ya kimataifa wa Hazina ya Marekani David Malpass.

Tangu benki hiyo ianzishwe mpaka hivi sasa Marekani k**a mwanahisa mkubwa wa benki ya dunia ndio humchagua rais wa benki hio.

Jim Yong Kim ametangaza kwamba ataachia madaraka ifikapo February 1. Alianza kuitumika benki hiyo k**a rais mnamo Julai, 2012. Mwaka 2017 aliteuliwa kwa tena kuwa rais wa benki hiyo.

Photos 13/01/2019

Azam FC wameichapa Simba SC 2-1 katika mechi kali ya fainali ya kombe la Mapinduzi ndani ya Uwanja wa Gombani uliopo Pemba, Zanzibar jioni hii.

Goli la kutangulia la Azam limefungwa kwa mkwaju mkali wa Mudathir Yahya dakika ya 44.

Simba wamesawazisha kupitia kichwa cha Yusuph Mlipili akimalizia kona ya Shiza Kichuya dakika ya 63.

Obrey Chirwa akaifungia Azam FC bao la pili akimalizia kwa kichwa krosi ya Nickolas Wadada dakika ya 72.

Kwa matokeo haya Azam FC ndiyo bingwa mpya wa kombe la Mapinduzi kwa mwaka 2019.

Photos 13/01/2019

Photos 13/01/2019

RATIBA YA MECHI ZA LEO JUMAPILI JANUARY 13.

Tanzania - Premier League
16:00 Biashara United Vs Coastal Union
16:00 Mbao Vs Stand United
16:00 Mbeya City Vs Mtibwa Sugar

Zanzibar - Mapinduzi Cup 2019(Fainali)
15:30 Simba SC Vs Azam FC

Africa - CAF Confederation Cup(Play-Off)
16:00 Gor Mahia Vs New Star
16:00 Jimma Kenema Vs Hassania Agadir
16:00 ZESCO United Vs Kaizer Chiefs
17:00 Bantu Vs Enugu Rangers
17:30 Cotonsport Vs Asante Kotoko
17:30 Otôho d'Oyo Vs KCCA
18:00 Ittihad Tanger Vs Zamalek
19:00 Al-Nasr Vs Salitas
19:30 Jaraaf Vs RSB Berkane
20:00 Al Hilal Omdurman Vs Mukura

England - Premier League
17:15 Everton Vs AFC Bournemouth
19:30 Tottenham Hotspur Vs Manchester United

Spain - La Liga
14:00 Atlético Madrid Vs Levante
18:15 Athletic Club Vs Sevilla
20:30 Barcelona Vs Eibar
22:45 Real Betis Vs Real Madrid

France - Ligue 1
17:00 Nantes Vs Rennes
19:00 Dijon Vs Montpellier
19:00 Toulouse Vs Strasbourg
23:00 Marseille Vs Monaco

Germany - Telekom Cup
15:00 Fortuna Düsseldorf Vs FC Bayern München
16

Photos 13/01/2019

Msimamo wa makundi ya Klabu bingwa barani Africa(CAF Champions League)baada ya kila timu kucheza mechi moja moja.

GROUP A
1. Wydad Athletic Club - WAC 🇲🇦 (3pts) +3
2. Lobi Stars Football Club 🇳🇬 (3pts) +1
3. Mamelodi Sundowns FC 🇿🇦 (0pts) -1
4. ASEC Mimosas 🇨🇮 (0pts) -3

GROUP B
1. Esperance du Tunis 🇹🇳 (1pt.) +0
2. Horoya AC 🇬🇳 (1pt.) +0
3. Orlando Pirates Football Club 🇿🇦 (1pt.) +0
4. Platinum Fc 🇿🇼 (1pt.) +0

GROUP C
1. TP Mazembe 🇨🇩 (3pts) +2
2. SC Constantin 1930 Herne-Mark e. V. 🇩🇿 (3pts) +1
3. Club Africain 🇹🇳 (0pts) -1
4. Ismaily S.C 🇪🇬 (0pts) -2

GROUP D
1. Simba SC Tanzania 🇹🇿 (3pts) +3
2. Al Ahly SC 🇪🇬 (3pts) +2
3. AS Vita Club 🇨🇩 (0pts) -2
4. JS Saoura 🇩🇿 (0pts) -3

Photos 13/01/2019

Kocha wa Yanga afurahishwa na hiki

Mwinyi Zahera ambaye ni Kocha Mkuu wa Yanga amefunguka kuwa anafurahishwa na sapoti ya mashabiki anayopata akiwa ndani ya Yanga hali inayomfanya afanye kazi kwa juhudi.

Zahera amesema mashabiki wa Tanzania ni tofauti na wa nchi ya Congo kwani kule kila ukanda una timu yake tofauti na ilivyo Tanzania.

"Mashabiki wanapenda mpira na wanapenda timu zao, wanazipa sapoti kwa hali na mali hali ambayo inanifanya niwe na furaha kuwa ndani ya Yanga na ardhi ya Tanzania," alisema Zahera.

Zahera amekuwa kipenzi cha mashabiki pamoja na wachezaji kutokana na namna anavyoibuka kifua mbele kwa kupindua matokeo kila anapozidiwa mbinu.

Photos 13/01/2019

Kiongozi Yanga atoa pongezi kwa Simba

Aliyewahi kuwa Ofisa Habari wa Yanga na hivi sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru amewapa pongezi Simba baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JS Saoura ya Algeria katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Muro ameandika hayo katika ukurasa wake wa Instagram ameeleza kuwa hatua waliyofikia Simba imewatoa kimasomaso watanzania wote baada ya ushindi huo.

"Tuna kila sababu ya kusimama pamoja k**a taifa na kuipongeza sana Simba, hakika mmetutoa kimasasomaso watanzania, ndugu yangu hongera, hamasa yako imekuwa chachu ya matokeo mazuri uwanjani. This Is Amazing And Fantastic" - alisema Muro

Aidha, Muro amempongeza Msemaji wa Simba, Haji Manara kwa namna anavyojitoa kutia hamasa na morali kwa mashabiki wa Simba na kuwa sababu au chachu ya matokeo mazuri.

Photos 12/01/2019

Mshambuliaji na nahodha wa Nkana FC ‘Red Devils’ Walter Bwalya anakaribia kujiunga na Simba kuziba nafasi itakayoachwa na Emanuel Okwi ambaye atajiunga na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

Bwalya atajiunga na Simba kwa mujibu wa kanuni na taratibu za Caf ambapo timu zilizofuzu hatua ya makundi ya mashindano ya Afrika hupewa fursa ya kuongeza wachezaji ili kuimarisha kikosi.

Photos 12/01/2019

Simba SC imekamilika, tutawashinda Waarabu - Waziri Mwakyembe

zikiwa zimesalia saa chache kwa Simba SC kuivaa JS Saoura katika mchezo wa klab Bingwa Afrika,Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kikosi cha Simba hivi sasa kimekamilika kila idara.

Akizungumza na kipindi cha Sport Leo kupitia Radio One ameeleza kuwa Simba imejiandaa vizuri
kuelekea mechi hiyo na ana imani itapata matokeo mazuri.

"Simba hii ya sasa imekamilika, naimani tutashinda mchezo wa leo dhidi ya waarabu," alisema Waziri Mwakyembe.

Leo majira ya saa 10 jioni Simba SC watashuka kwenye dimba la uwanja wa taifa kuivaa JS Saoura kutoka nchini Algeria, katika mchezo huo Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

11/01/2019

Full Time: Azam FC 3-0 KMKM

9' 62' 81' Moris, Sure Boy, Chirwa ⚽⚽⚽

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Mwanza?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Website

Address


Mwanza