Naipenda YANGA YANGU

Naipenda YANGA YANGU

Share

True fans of young Africans kwa washabiki wa kweli

17/03/2026

WANANCHIIIIIIIII

Naombeni mpeni support huyu mwana Dada katika page yake ya Michezo Link nawawekea hapo chini ni mtoa taarifà za Michezo za uhakika kwa wakati...!¡! Tafadhali ñaombeni mumpe support zenu🙏💚

Link hii hapa 👇

https://www.facebook.com/profile.php?id=100083670391800

10/04/2024

Tarehe 20 Yupo wakuu.

Si wenyewe mnaona kaingia kupasha misuli😀

Follow 𝐓𝐞𝐚𝐦 𝐨𝐟 𝐂𝐢𝐭𝐢𝐳𝐞𝐧𝐬

16/11/2023

HEE !!! MIAKA 15 ?

Nimfash Berchimas mwenye umri wa miaka 15 ndiye mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kuiwakilisha na kuifungia Marekani kwenye Kombe la Dunia la Wanaume U17 tangu Freddy Adu mwenye umri wa miaka 14 kufanya hivyo mwaka wa 2003.

2003 : Freddy Adu alifunga mabao manne katika michezo yake miwili ya kwanza kwenye Kombe la Dunia la U17

2023 : Nimfash Berchimas afunga mabao matatu katika mechi zake mbili za kwanza kwenye Kombe la Dunia la U17

[Chanzo : BR Football]

Follow Team of Citizens

06/10/2023

Habari kubwa sasa kwenye Social Media ni Group Stage ya Champions League. Na 70% ya watu wanajadili kuhusu Kundi letu Wananchi .. 👊

Hii inatoa picha ni kwa Jinsi Gani Brand ya YangaSc ni kubwa na Inavutia wengi kuizungumza..

Ni nzuri hii Lakini kwa sasa, ombi Langu kwa Mashabiki na Wanachama tusiingie kwenye mtego wa kuiwaza Novemba wakati Oktoba bado Hatujaimaliza.

Hatua ya Makundi itaanza Novemba .. Lakini kesho, Oktoba 7 hapa CCM Kirumba Tuna Jambo zito kweli kweli.

Tuna mchezo mgumu wa kuzisaka Pointi 3️⃣ dhidi ya timu ngumu ya Geita Gold .. Tuweke Focus yetu hapa kwa sasa.

Yoyote atakayeanzisha mjadala wa Group Stage kwenye kundi Lolote la WhatsApp.. Mwambieni Asubiri kwanza .. YangaSc Inashida na hizi pointi 3️⃣ za Kesho

Dua, hamasa ziwekwe hapo .. Tukijielekeza mno kuijadili Group Stage itafanya tuingie kesho tukiwa hatuko 100% na umakini mbele ya Geita ..

Tulimalize hili la kesho Wananchi .. 👊 Mengine yatafata.

✍️ Team of Citizenss

06/10/2023

24/25 Nov: CR Belouizdad - Away
ALGERIA

1/2 Dec: Al Ahly - Home
DSM

8/9 Dec: Medeama - Away
GHANA

19 Dec: Medeama - Home
DSM

23/24 Dec: CR Belouizdad - Home
DSM

1/2 Mar: Al Ahly - Away
EGYPT

06/10/2023

AL AHLY 🇪🇬
CR BELOUIZDAD 🇩🇿
YOUNG AFRICANS 🇹🇿
MEDEAMA SC 🇬🇭

Hili ndilo group la young africans mabingwa wa Tanzania 🇹🇿 wananchi tuna kazi muhimu na ngumu ya kufanya kuhakikisha tuna fuzu kwenda hatua ya robo final



06/10/2023

"Nafahamu kesho tutakuwa na mchezo mgumu na sijui hali ya Uwanja ikoje lakini nafikiri itakuwa k**a Uwanja wa mchezo wetu uliopita.
Ukweli nina wasiwasi sana na viwanja pamoja na maamuzi ya waamuzi uwanjani nina imani kutakuwa na mabadiliko kwenye hili kwasababu kila kitu kinaonekana wazi"

Maandalizi kwa upande wetu siyo mazuri sana kutokana na ratiba lakini sisi ni wataalamu na ligi kuna muda inakuwa na ratiba ngumu lazima kuwa tayari. Leo tutakuwa na mazoezi jioni, ambayo yatatusaidia kuona hali ya wachezaji kuelekea mchezo wetu wa kesho dhidi ya Geita Gold"


02/10/2023

“Kutoka mwaka 1998 hadi sasa [2023] ni miaka 25, ni umri wa kijana ambaye tayari anaweza kuwa kwenye ndoa. Ni miaka mingi sana, wakati Yanga inacheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya mwisho mimi nilikuwa bado nipo shule.”

“Mapenzi ya Yanga yalikuwa ndani ya familia yetu, nakumbuka siku hiyo mzee na familia yote tulishangilia sana Yanga kufuzu hatua ya makundi. Kwa hiyo Yanga kufuzu hatua ya makundi baada ya miaka 25 ni zawadi kwa familia yangu kwa sababu hata wao walitamani kuiona tunairudisha Yanga hatua hizi.”

“Na mimi nimefurahi sana kuona jambo hili limetimia, tunachotakiwa kufanya ni kuhakikisha hatua hizi tunakuwa wenyeji kwa kushiriki kila msimu.”

- Arafat Haji [], Makamu wa Rais Yanga.

30/09/2023

JOYCE LOMALISA MUTAMBALA, ilikuwa ni siku ya Stephen Aziz Ki kwenye vichwa vya Mashabiki wa Yanga ila uwanjani ilikuwa siku ya Mkongoman, aliyeubadili mpira k**a mziki wa Kanda Bongo Man, Juma Aweso anaweza kuwa Waziri wa Maji ila awe makini Zuhra Yunus anaweza kuachia press kuwa yeye ndie Mteule mpya wa Rais.

Wanasema Sudan kuna vita lakini dakika 90 za mchezo waliweka silaha chini, kumtazama Mwanaume huyu akiamrisha Wanamgambo, alipageuza Chamazi k**a Darfur, pass zilipigwa k**a mabadilishano ya risasi dhidi ya Wanamgambo, Gaidi wa mbinu za Garmondi, football is simple right? Look at him he doesn’t use right foot.

Get ready to rumble kwa sauti ya Michael Buffer, miguso k**a beat za S2Kizzy, 13 mgongoni k**a Michael Ballack asiye na bahati na fainali ila 13 yake ina bahati na hizi hatua kubwa, laana na mkosi hazivuki bahari, anaweza kuwa anamalizia mkataba wake ila bila shaka atastaafu kwa ufahari.

The epic night of Champions League football is back, Wananchi wamepanda chat! All the best.

29/09/2023

》》Kocha Mkuu Wa Timu Ya Wananchi Miguel Gamond Kuhusu Ubora wa Kikosi Cha Yanga,

🗣️“Nafurahi kufanya kazi na Yanga ina wachezaji wengi wazuri na wote Wana uchu wa mafanikio hiyo ndio inaweza kuwa siri ya Matokeo mazuri ambayo tumekuwa tukiyapata ndani ya Uwanja,

“Hatuna mchezaji tegemezi kila mchezaji anatumika kutokana na ushawishi wake mazoezini, kuhusu Uwezo kwa asilimia kubwa Wote wana Uwezo Sawa,

“Kinachotofautisha ni aina ya uchezaji na kila mmoja anatumika kutokana na aina ya mpinzani tunayekutana naye.” -Amesema Gamond 🔰💪🏾

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Mwanza?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Website

Address


Lamadi
Mwanza
0001