09/03/2026
K**A KUNA NYAKATI MUHIMU SANA MASHABIKI WA ARSENAL WANAPASWA KUUNGANA BASI KIPINDI HIKI
"unganeni hakuna mtu anaipenda Arsenal zaidi yenu wenyewe"
nyakati hizi ambazo wachezaji wanapambana kwa jasho na damu kulipigania kombe ambalo ni kiu ya mda mrefu kwa timu husika na mashabiki kwa ujumla
"eleweni kwamba hata ikitokea ghafla timu ikipoteza mechi basi msitoke kwenye reli hakuna mtu anawatakia mazuri"
NIMESIKIA HIZO AGENDA ZINASEMA TIMU HAICHEZI MPIRA MZURI
"nafikiri mnapaswa kutambua nyendo za haters"
sasa k**a timu haichezi mpira mzuri si ndo utafute timu ambayo inacheza mpira mzuri uangalie mechi zao kwani lazima Arsenal?
kwa sababu hii kauli ukiichunguza unagundua haina mashiko imekaa kichuki zaidi haswa walipogundua kua kuna possibility kubwa ya Arsenal kubeba hili kombe la Epl
kwanza mashabiki wa Arsenal ndio mjue kumbe Arsenal ni ICON ya mpira mzuri pale nchini England licha ya kwamba hawaipendi ila wakikaa kwenye runinga wanafaidi burudani
"hata wasipokiri tayari ukweli unadhihiri kupitia hii milio yao"
EPUKENI HUU MTEGO WANALENGA KUWATENGANISHA MAZIMA
"kiufupi wanacheza na akili zenu mashabiki"
halafu tazama hao Legends wa vilabu tofauti wameungana kuishambulia Arsenal kwa maneno mabaya ambayo yanalenga kuwakatisha tamaa wachezaji lakini sidhani k**a agenda zao zitafua dafu
kwanza mashabiki wa Arsenal mkae mkijua kwamba kwa sasa Arsenal ni bonge moja la CONTENT kwa hiyo watu wanatumia fursa kutafuta like,comment na viewer
wanaamini kwamba ukiongelea Arsenal zaidi kwa mabaya basi utapata attention na hapa simaanishi kwamba wanatakiwa waiseme kwa mazuri yani sipo hapa kumpangia mtu cha kusema
"ila jiulizeni kwa nini timu ikifanya vizuri wanapiga kimya hawatoi credit wanabaki kuzusha lolote lenye udhaifu ilimradi iwe mada?"
* magoli ya kona
* mpira mbovu
* hawana world class player hata mmoja
* wakibeba kombe itakua ni msimu mbovu zaidi
* k**a wakibeba Epl tu wasipobeba UEFA watakua wamefeli msimu huu
"yaani mfululizo wa kauli mbovu sana mtu akipewa kipaza anatema nyongo ya chuki"
SASA NIMALIZIE KWA KUWASISITIZA MASHABIKI WA ARSENAL
mashabiki wa Arsenal hakuna mtu atakuja kuwakumbusha kuipenda timu yenu zaidi ya nyinyi wenyewe kumbukeni wao timu zimevurugwa hazina muelekeo na hawasemi hadharani wapo bize kuisema Arsenal
kutwa wanazipamba timu zao na kila kitu wanaitumia Arsenal k**a kipimo cha ubora wao
"sasa k**a Arsenal haina cha maana kwao mbona kwa nini waitumie k**a SI unit kwenye comparisons zao?"
NOTE: siku zote ukikaribia kuyafikia mafanikio basi jiandae kusikia milio kutokea kila pembe
"AHSANTENI"