Vitimbi vya soka

Vitimbi vya soka

Share

💥SOTE TUFURAHI NA SOKA LETU

Whatsapp +255 676167186

17/04/2026

💥Iniesta kuhusu Ronaldinho kuelekea El clasico:

"Kabla ya mechi ya El Clasico dhidi ya Real Madrid, Ronaldinho alinipigia simu usiku wa manane. Nilivyopokea simu akaniambia:

'Andres, najua ni saa 9 tisa usiku, lakini sina budi kukuambia kitu:
Andres nitaondoka mwezi wa sita, kaka yangu tumefikia makubaliano ya hali ya juu na Real Madrid, wametoa hela kubwa ambayo siwezi kukataa, wewe ni mdogo na unaweza kunielewa, lakini tafadhali usiseme chochote kwenye chumba cha kubadilishia nguo au kwa uongozi, usinisaliti, ninakuamini zaidi kuliko mtu mwingine yeyote, Andres.'

Sikulala usiku kucha, ukweli sikuweza kuelewa kwamba anatuacha vipi na kwenda timu nyingine, haswa kati ya timu zote kwanini achague mpinzani wetu mkuu Real Madrid ...😠

Siku ya El Clasico ilipofika katika chumba cha kubadilishia nguo cha Santiago Bernabeu, na tulipokuwa tukibadilisha nguo zetu, Ronaldinho alisimama na kuanza kusema:

'Jamani, leo tuna mchezo muhimu, tutacheza dhidi ya timu imara, lakini siku hizi nimegundua kuwa sisi ni k**a familia kubwa. Niliwapigia ninyi nyote usiku wa manane kusema kwamba ninaondoka mwezi wa sita, lakini hakuna hata mmoja wenu aliyetoa siri, Nitakuwa hapa kwa miaka mingi zaidi, na sasa twendeni uwanjani tukawafundishe soka hawa watu wa Madrid.'💪

kumbe ile Ilikuwa mbinu ya uhamasishaji, ambayo ilikuwa na lengo maalum kwa Ronaldinho. Baada ya kile kilichotokea, nilielewa kuwa tulikuwa tayari kufia ndani badala ya kusalitiana.

Katika mechi hiyo ya El Clasico alifunga mabao mawili, na uwanja mzima wa Santiago Bernabeu walisimama kumpigia makofi👏, huyo alikuwa Ronaldinho." 🔥

💥K**a uliwahi kusikia stori kuhusu Ronaldinho kupigiwa makofi na uwanja mzima hata mashabiki wa upinzani (Real Madrid) basi ndio ilikuwa mechi hiyo👏.

16/03/2026

💥Wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza mwaka 2006 kati ya Chelsea na Reading, mlinda mlango wa Chelsea Petr Cech alipata jeraha la kichwa kufuatia teke la kichwa la mchezaji wa Reading Stephen Hunt.

Carlo Cudicini ambaye alikuwa ni kipa namba mbili alitakiwa aingie lakini pia akaumia na hivyo John Terry alitoka kwenye nafasi ya beki na kwenda langoni katika dakika za mwisho za mchezo na akaisaidia Chelsea kushinda 1-0.

Baada ya tukio hilo, Cech alilazimika kuvaa vazi kichwani la kujikinga katika michezo iliyofuata.

Umewahi kupewa stori gani kuhusu vazi la kichwa la Peter Cech?😂😂

08/03/2026

💥Luis Nani🇵🇹:

"Siku moja, Alex Ferguson alituuliza k**a kuna mtu angeweza kumrudisha nyumbani baada ya mchezo dhidi ya Fulham. Nikasema: 'Mimi bosi, nitakupeleka nyumbani, bila wasiwasi!' Kisha kwenye huo mchezo ilikuwa 2-1, tukapata penati na nikamuomba Giggs aniruhusu nipige, akakubali ila nilivyopiga nikakosa penati ile😁

Fulham wakasawazisha na kufanya iwe 2-2 katika dakika ya 88... Baada ya mchezo k**a tulivyopanga nikamchukua Sir Alex Ferguson nyumbani lakini hakuzungumza namimi njia nzima." 😅

K**a wewe ungekuwa ndio Ferguson ungekuwa katika hali gani kwenye hilo gari la Luis Nani😂.

01/03/2026

💥Mwaka 1978, Ajax walikuwa na mechi ya kumuaga Johan Cruyff, ambapo waliwakaribisha Bayern Munich.

Baada ya mechi, Johan Cruyff alisema: "Bayern waliingia uwanjani k**a wapiganaji, kana kwamba wanacheza fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya. Ilikuwa ni aibu kubwa na dharau kabisa." 👀🔥

Bayern Munich walishinda 8 - 0🙌😂😂😂.

28/02/2026

💥Orlando Pirates walikuwa wanaongoza 1-0 dhidi ya Baroka mpaka dakika za lala salama katika mchezo wa Ligi Kuu ya Absa ya Afrika Kusini Novemba 2016.

Baroka walipata kona dakika ya 95 na kipa wa Baroka, Oscarine Masuluke, akasogea kushambulia na kuisaidia timu yake kupata bao la dakika za mwisho.

Masuluke alifunga bao la kusawazisha kwa kubinuka (Tikitaka) na kufanya matokeo kuwa 1-1.

Bao hilo lilimaliza la pili, nyuma ya bao la scorpion la Olivier Giroud, katika orodha ya Tuzo ya Puskas(Goli bora la mwaka duniani).🙌🙌🔥

26/02/2026

💥Kamera zilikuwa zikiwanasa mara nyingi wakiishangilia kwa pamoja katika klabu ya Uturuki ya Fenerbahçe, na wakawa k**a moja ya kielelezo cha mapenzi ya kweli ndani ya mchezo wa soka, Wapenzi hao ni Muhtasham na mkewe, Ihsan.

Mwaka 2015, Muhtasham alionyesha dalili za ugonjwa, lakini bado alihakikisha anahudhuria mechi za Fenerbahçe na Ihsan, ambaye alikuwa na uwezo wa kusimulia kila kitu kinachotokea baada ya mechi.

Mwaka 2016, Ihsan alikaa peke yake kwenye zile siti baada ya Muhtasham kufariki, aliendelea kuhudhuria mechi bila kukosa, licha ya huzuni kubwa aliyokuwa nayo.

Mwaka 2020, Ihsan naye alifariki, Waliacha viti vyao vikiwa tupu, Mashabiki kwa kuheshimu uwepo wao wakaeka picha zao kwenye zile siti walizokuwa wamezoea kuwaona wakiwa pamoja wamekaa.

Ihsan na Muhtasham… hadithi yao ya mapenzi haijafutika mpaka leo katika uwanja wa Fernerbahçe❤️.

22/02/2026

💥🇸🇪 Ibrahimovic:

"Nilivyokuwa Juventus tulicheza dhidi ya Inter. Materazzi alinichezea rafu mbaya k**a vile muuaji na kuniumiza. Miaka minne baadaye, alinijia na nikampiga kwa taekwondo. Nilimpeleka hospitali. Stankovic aliniuliza: ' kwa nini ulifanya hivyo?' Nilimwambia: 'Nimekuwa nikingojea hii nafasi kwa miaka minne.'" 😂🙌

Zlatan kisasi katoka nacho Juventus kaja kulipa kipindi yupo Ac Milan🙌🙌😂😂😂.

20/02/2026

💥JE, WAJUA

Ufaransa ilifungana 1-1 na Korea Kusini kwenye Uwanja wa Leipzig Arena katika Kombe la Dunia mwaka 2006 nchini Ujerumani. 👀

Zinedine Zidane alikasirishwa na matokeo na akaugonga kwa nguvu mlango wa chumba cha kubadilishia nguo wakati wanarudi mechi ilipoisha.

Mpaka leo utawala wa Leipzig haujarekebisha mlango ambao Zidane aliugonga, lakini badala yake wameweka fremu ya dhahabu karibu na eneo alilogonga ili kuweka k**a kumbukumbu kwao kwa mchezaji huyu.

Haya ni zaidi ya mapenzi kwa Zidane❤️🙌🙌

16/02/2026

💥Ujumbe wa Ibrahimović kwa Carlo Ancelotti😂:

"Habari Carlo, hongera kwa kila kitu ambacho umefanikisha, umeshinda yote na unastahili kuitwa kocha bora zaidi duniani. Nilikuwa na bahati ya kucheza chini yako, lakini usisahau, ulikuwa na bahati kuwa namimi pia."😂

"Kitu kikubwa zaidi kwangu hakikuwa kufanya kazi na wewe k**a kocha tu, bali kukufahamu k**a mtu. Kusema kweli, wewe ni mtu bora zaidi kuliko kocha. Ninakupenda Carlo, lakini tafadhali usiniombe nikukopeshe pesa tena, inaonekana k**a unaendelea vizuri sasa hivi!" 😂.

Huyu mtu hajaacha bangi kabisa😂😂😂.

11/02/2026

💥Valverde🇺🇾:

"Nilikuwa namkimbiza Morata ila kila nikijaribu kumshika nilishindwa...
Na ghafla nikasikia sauti nyuma yangu, k**a sauti ya watu 100 wakipiga kelele juu ya mapafu yake!
Sauti hiyo ilikuwa ikiniambia "Muue...." Ilikuwa ni sauti ya Sergio Ramos 😂
Baada ya hapo kilichobaki ni historia🙌.

Hii ni kadi nyekundu bora katika historia ya soka.
Na baada ya hapo, Real Madrid walitwaa taji 🏆”.

30/12/2025

💥HII KALI🙌😂

Tangu atue England, Christian Benteke alikuwa akiwafunga sana Liverpool karibu kila msimu. Ili Liverpool wamzuie waliamua kumsajili kwa pauni milioni 50.

Alikaa msimu mmoja tu Anfield, akifunga mabao 9 tu, kabla ya kuuzwa Crystal Palace.

Katika msimu wake wa kwanza akiwa na Palace, alirudia yake yale, alifunga bao mbili dhidi ya Liverpool kwenye Uwanja wa Anfield na kuiongoza Palace kushinda 2-1 😁⚽.

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Website

Address


Dar Es Salaam