VETA

VETA

Share

This is an official account for the Vocational Education and Training Authority (VETA).

Photos from VETA's post 19/07/2026

Wanufaika wa mradi wa Dumisha Amani wahamasishwa kuomba zabuni za Serikali

Mkuu wa wilaya ya Kigoma, Dkt. Rashid Chuachua, amewahamasisha wanufaika wa mafunzo ya ufundi kupitia Mradi wa Dumisha Amani chini ya ufadhili wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Amani na Maendeleo (UNPDF), Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), China Petroleum Pipeline (CPP) kwa kushirikiana Global Peace Foundation (GPF) Tanzania, kuomba zabuni za Serikali kupitia vikundi watakavyojiunga ili waweze kujitegemea.

Chuachua ametoa wito huo tarehe 18 Julai 2026 katika viwanja vya chuo cha Ufundi Stadi na Huduma cha Mkoa wa Kigoma (chuo cha VETA Kigoma) wakati wa hafla fupi ya kufungwa rasmi kwa mafunzo ya Dumisha Amani yaliyotolewa kwa muda wa majuma mawili chuoni hapo.

“Niwatie shime ninyi mnaohitimu leo kujiunga kwenye vikundi ambavyo vitawafanya msajiliwe na mfahamu namna ya matumizi bora ya mfumo wa Serikali wa ununuzi (NeST) ili muweze kuomba zabuni za Serikali ili na nyinyi muweze kupata fursa za kiuchumi na kujitegemea,” alisema Chuachua.

Aidha kwa upande mwingine Chuachua amewakumbusha vijana hao uwepo wa fursa za mikopo kutiko Serikalini isiyokuwa na riba kwa vikundi lakini pia kwa mtu mmojammoja mwenye ulemavu.

Kwa upande wake Afisa Maradi kutoka UNDP-Tanzania Josephine Sepeku amesema katika vyuo 4 ambavyo vimehusika kutoa mafunzo kupitia mradi wa Dumisha Amani kila chuo kitapatiwa dola 42,000 sawa na shilingi 110,748,120 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha vijana (Youth centre) ili vijana katika maeneo hayo waendelee kunufaika na ujuzi walioupata.

Kwa upande wake Alphoncina Mashana, Afisa Mkuza Mitaala Mwandamizi kutoka VETA Makao Makuu amewataka vijana hao kwenda kutumia kikamlifu ujuzi walioupata aidha kwa kujiajiri, kuajiri wengine au kuajiriwa ikiwa ni pamoja na kudumisha amani katika maeneo yanayowazunguka.

Akitoa taarifa fupi, Mkuu wa Chuo cha VETA Kigoma Mhandisi Paulo Kimenya amesema mafunzo hayo yalianza rasmi tarehe 6 Julai 2026 kwa muda wa wiki mbili yakiwa na jumla ya washiriki 60, wanawake 38 na wanaume 22.

Amesema mafunzo yamehusisha stadi nne ambazo ni Ubunifu, Ushonaji na Teknolojia ya Nguo, Ufundi Bomba, Mapishi na Umeme wa Majumbani

Naye Amina Issa kwa niaba ya wahitimu wenzake amesema mafunzo hayo yamewajengea uwezo wa kutambua fursa za kiuchumi zilizopo katika jamii, kuanzisha shughuli za uzalishaji mali, kufanya kazi kwa ushirikiano kupitia vikundi vya ujasiriamali, pamoja na kujenga utamaduni wa amani, mshikamano na uvumilivu katika jamii yao.

18/07/2026
Photos from VETA's post 17/07/2026

VIJANA 100 MTUMBA WANUFAIKA NA PROGRAMU YA MAMA SAMIA YA URASIMISHAJI WA UJUZI

Jumla ya vijana 100 kutoka Jimbo la Mtumba, jijini Dodoma, wamekidhi vigezo na kutunukiwa vyeti vya Utambuzi na Urasimishaji wa Ujuzi (Recognition of Prior Learning–RPL) kupitia Programu ya Mama Samia inayotekelezwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).

Akizungumza katika hafla ya utoaji vyeti tarehe 16 Julai, 2026, Mbunge wa Jimbo la Mtumba ambaye pia ni Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha programu hiyo inayowatambua rasmi Watanzania waliopata ujuzi nje ya mfumo rasmi wa elimu na mafunzo.

Amesema hatua hiyo inawawezesha mafundi wenye uzoefu kuthibitisha umahiri wao kwa vyeti vinavyotambulika rasmi, hivyo kuongeza fursa za ajira na kujiajiri.

Amewataka wahitimu kutumia vyeti hivyo kuongeza thamani ya ujuzi wao na kuwahamasisha vijana wengine kushiriki katika programu hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore, amesema lengo la programu hiyo si kutoa vyeti pekee, bali kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji na kuchangia ukuaji wa uchumi.

Amesema urasimishaji wa ujuzi unaendana na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ya kujenga taifa lenye watu wenye ujuzi na ubunifu.

Aidha, amemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kuwekeza katika elimu ya ufundi stadi, akieleza kuwa Serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni 100 kwa ujenzi wa vyuo vipya 65 vya VETA nchini. Pia aliwahimiza vijana kutumia fursa ya asilimia 30 ya zabuni za umma zinazotengwa kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.

Kwa upande wake, Meneja wa Mitihani na Utunuku wa VETA, Bwire Aly, amesema programu hiyo ililenga kuwafikia vijana 14,400 katika mikoa 11, lakini hadi Mei 2026 zaidi ya washiriki 18,000 walikuwa wamejitokeza kufanyiwa tathmini ya ujuzi.

Amesema katika Jimbo la Mtumba waombaji 186 walijisajili, huku washiriki 100 wakifanyiwa tathmini na wote kufaulu katika fani mbalimbali za ufundi stadi, hivyo kutunukiwa vyeti vya utambuzi na urasimishaji wa ujuzi.

17/07/2026

Ziara ya Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania,
Mhe. Eunju Ahn, ametembelea Chuo cha VETA Dodoma kujionea hali ya utoaji mafunzo ya Ufundi Stadi, Tarehe 16 Julai, 2026.

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Address


VETA Head Office, 12 VETA Road, 41104 Tambukareli, P. O. Box 802, Dodoma Tanzania, Email: Info@veta. Go. Tz Telephone: +255 26 2963661 Fax: +255 22 2863408 Url: Www. Veta. Go. Tz
Dodoma
PLOTNO.18

Opening Hours

Monday 07:30 - 21:30
Tuesday 08:00 - 21:30
Wednesday 07:30 - 21:30
Thursday 07:30 - 21:30
Friday 07:30 - 21:30